July 31, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Jeshi la Polisi latoa tahadhari Simba na Yanga

Spread the love

 

 JESHI la Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam limesema kuwa limejipanga kuimalisha ulinzi, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga utakaopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo utaanza majira ya saa 11 jioni, Tarehe 3 Julai 2021, ambapo klabu ya Simba ndio watakaokuwa wenyeji wa mchezo.

Taarifa kutoka ndani ya jeshi hilo imeeleza kuwa, wamejiapanga kuweka Askari wa kutosha katika kila eneo ndani ya Uwanja huo.

Mechi hiyo ambayo inavuta hisia za mashabiki wengi wa mchezo huo nchini, kutokana na ukubwa wa klabu hizo ndani ya Tanzania.

Aidha Polisi wametoa zuio kwa mashabiki kuingia Uwanjani na chupa ya Maji au kinywaji chochote, silaha pamoja na mashabiki kukaa sehemu ambapo tiketi zao haziwaruhusu.

Pia jeshi la polisi limetoa tahadhari kwa watakao kwenda na watoto Uwanjani, kuwanao karibu au kutumia busara kwa kuwaacha nyumbani.

Huu utakuwa mchezo wa kufunga dimba kwenye mzunguko wa Pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kwa msimu wa 2020/21, kwenye mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka kwa kufungana bao 1-1.

error: Content is protected !!