May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jeshi la Polisi latoa masharti matano mchezo Simba na Yanga

Spread the love

 

JESHI la Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam limetoa masharti matano kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga ikiwemo kutaka mashabiki kuepuka mihemko ya maneno ya kuhasimiana wakati mchezo huo unaendelea. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo utafanyika siku ya Jumamosi majira ya saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habaru hii leo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa jeshi hilo limejipanga kuimalisha ulinzi siku ya mchezo huo katika maeneo yote ya Uwanja zikiwemo barabara za kuingia na kutoka Uwanjani hapo sambamba na kutoa masharti kwa mashabiki watakaokwenda kuangalia mchezo huo.

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa

 

“Hatutaruhusu mashabiki kuingia na chupa za maji uwanjani kwa kuwa hutumiwa kurushiana pale timu moja inapokuwa haikubali matokeo sambamba na kutoruhusu kuingia na Silaha ambayo inaweza kugeuka kuwa hatari” alisema Mambosasa

“Hatutoruhusu kupaki magari ndani ya Uwanja na magari yatakayo ruhusiwa ni yenye vibari maalumu na pia hatutoruhusu kukaa sehemu ambao tiketi yako haikuruhusu kukaa naomba uheshimu hali yako” alisema Kamanda huyo

Aidha jeshi hilo limetoa tahadhari kwa wazazi watakaokwenda na watoto Uwanjani siku ya mchezo huo kuwa makini na kujiepusha kukaa sehemu zenye msongamano.

Mchezo huu unakutanisha timu ambazo zipo juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo Simba ipo kwenye nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 61 mara baada ya kucheza michezo 25, huku nafasi ya pili wakiwa Yanga wenye pointi 57 mara baada ya kucheza michezo 27.

error: Content is protected !!