Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Jeshi la Polisi lamshangaza Mbowe
Habari za Siasa

Jeshi la Polisi lamshangaza Mbowe

IGP, Camilius Wambura
Spread the love

 

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuendelea kulinda mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa vya upinzani, huku akiwaahidi Askari Polisi kwamba chama chake kikiingia madarakani kitaendelea kulinda maslahi yao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Njombe … (endelea).

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Chadema, uliofanyika tarehe 27 Februari 2023, mkoani Njombe, Mbowe amesema Jeshi la Polisi kwa sasa limebadilika kwa kuwa na utu dhidi ya vyama vya upinzani, tofauti na ilivyokuwa miaka saba iliyopita.

“Tunawaahidi Polisi siku chama chetu kitaongoza dola, hatutaagiza Polisi kutoka Congo au Kenya, ni ninyi ambao vijana wetu mtakaoendelea na wajibu wenu. Msiipendelee Chadema, wala chama chochote cha siasa. Simameni katika kweli na haki,” amesema Mbowe.

Amedai kuwa, mabadiliko hayo yanatokana na kiongozi aliyekuwa madarakani kukomesha vitendo vya kikatili.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

“Ndani ya wiki moja tumezunguka kufanya mikutano ya hadhara, nikiangalia jeshi la polisi silielewi, najiuliza hivi jeshi hili lenye ubinadamu huu ndiyo lilelile lililokuwa miaka saba iliyopita? Au limebadilika, hii maana yake kiongozi wa taifa sio jambo la masihara, mkiwa na kiongozi mkatili anatengeneza mfumo mzima wa ukatiili,” amesema Mbowe na kuongeza:

“Kwa miaka saba iliyopita tuliwaona adui wa taifa letu, tumetembea kote hakuna wa kutusumbua. Wametusindikiza wameonyesha ushirikiano bila ubaguzi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!