Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Jeshi la Polisi kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika utafiti
Habari MchanganyikoTangulizi

Jeshi la Polisi kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika utafiti

Dk. Lazaro Mambosasa
Spread the love

 

JESHI la Polisi Nchini limesema kuwa katika kukabiliana na mabadiliko ya sayansi na technolojia limepanga kuja na mkakati wa Pamoja kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika maswala ya tafiti mbalimbali ambazo zimelenga kubaini na kukomesha vitendo vya kiharifu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akiongea na waandishi wa Habari Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi , SACP Dk. Lazaro Mambosasa amesema moja ya majukumu yao ni kulinda rai ana mali zao ambapo amebainisha kuwa kupitia kitengo cha utafiti ndani ya Jeshi hilo na katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam wameona vyema wafike chuoni hapo ili kujifunza maswala mbalimbali katika tafiti.

Aidha SACP Dk. Mambosasa amewambia waandishi kuwa malengo ya Mkuu wa Jeshi hilo IGP Camillus Wambura ni kuona Jeshi la Polisi linawekeza katika tafiti ambapo amebainisha kuwa Jeshi hilo limepanga kuingia makubaliano baina ya chuo cha taaluma ya Polisi Dar es salaam Pamoja na chuo kikuu cha Dar es salaam katika kufanya tafiti.

Nae Kamishina Msaidizi wa Polisi ACP Ralph Meela ambae ni Mkuu wa Kituo cha Utafiti cha Jeshi la Polisi kilichopo Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam amesema kuwa kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia wameona vyema waje na mtazamo mpya katika kutanzua mbinu zinazotumiwa na wahalifu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

error: Content is protected !!