June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jeshi Burundi lamng’oa Nkurunziza

Waandamaji wa Burundi wakishangilia pamoja na wanajeshi mjini Bujumbura, baada ya kutangazwa kuwa Pierre Nkurunziza kupinduliwa

Spread the love

PIERRE Nkurunziza, Rais wa taifa la Burundi, amepinduliwa na kikosi cha jeshi la nchi hiyo. Mapinduzi hayo yamefanyika wakati Nkurunziza akiwa jijini Dar es Salaam, alikokuwa akihudhuria mkutano kuhusu taifa lake. Anaripoti Saed Kubenea … (endelea).

Meja Jenerali Godefroid Niyombare, amelitangazia taifa kupitia radio na televisheni binafsi, kwamba “Rais Nkurunziza amepinduliwa” na kutangaza kuundwa kwa Kamati Maalum ya watu sita kuongoza nchi.

Mapinduzi dhidi ya utawala wa Nkurunziza yamefanyika katika kipindi ambacho kiongozi huyo alikuwa mbioni kugombea kipindi cha tatu madarakani, jambo ambalo lilipingwa na baadhi ya vyama vya upinzani na maofisa wa jeshi.

Meja Jenerali Niyombare amenukuliwa akisema, mapinduzi hayo yamefanyika ili kuirejesha nchi katika umoja. Akamtuhumu Rais Nkurunziza kubomoa umoja wa kitaifa katika nchi; udikteta, matumizi mabaya ya madaraka na kutoheshimu makubaliano ya amani ya Arusha.

Habari zinasema, mara baada ya tangazo la mapinduzi kutolewa, mamia ya wananchi waliandamana mjini Bunjura kuunga mkono mapinduzi hayo, huku waandamanaji wakiwa takriban kilomita moja kutoka kwa kasri ya rais.

Hata hivyo, wanajeshi wanaomuunga mkono Nkurunzinza bado hadi saa 12 jioni ya leo, walikuwa wanadhibiti Ikulu na kituo cha redio ya taifa.

Katika hatua nyingine, ndege ya Rais Nkurunziza, imezuiwa kutua nchini mwake na huenda imeaelekea nchini Uganda.

Hata hivyo, taarifa nyingine zinadai kuwa Rais Nkurunziza amerejea jijini Dar es Salaam baada ya kushindwa kutua Bujumbura.

Ikiwa jarbio la mapinduzi dhidi ya Rais Nkurunziza litakuwa limefanikiwa, basi itakuwa pigo kubwa kwa mahafidhina katika eneo hili la Afrika Mashariki. Rais Nkurunziza alikuwa swahiba mkubwa na Rajabu Hussen ambaye alikuwa katibu mkuu wa chama tawala.

error: Content is protected !!