July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jerry Silaa awakacha waandishi

Jerry Silaa

Spread the love

MEYA wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, amewakimbia waandishi wa habari aliowaita kuzungumza nao ofisini kwake, Ilala, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Sarafina Lidwino … (endelea).

Silaa ambaye ni diwani wa kata ya Gongo la Mboto, alipanga kukutana na waandishi wa habari, katika ofisi za umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM).

Wito wa Silaa kukutana na waandishi wa habari ulipitia kwa waafuasi wake mbalimbali kwa ajili ya mazungumzo ambayo hayakuwekwa wazi.

Waandishi hao walitakwa kufika ofisini hapo saa 09:00 asubui, lakini walikalishwa ofisini hapo hadi saa 10:35   pasipo muhusika kutokea eneo la tukio.

Waandishi hao, walianza kuja juu, na baadhi kuondoka eneo hilo la tukio, baada ya kuona hakuna kinachoendelea, zaidi ya kupoteza muda wao, ITV ndio walikuwa wa kwanza kuondoka eneo la tukio baada ya kujua hakuna lolote linaloendelea.

Baada ya waandishi kuchoshwa na mazingira hayo, ndipo baadhi wakamtafuta mmoja kati ya wafuasi wa Silaa ambaye aliyehusika kuwapigia simu baadhi ya waandishi, na kuanza kumlalamikia, huku wakihoji kama muhusika anakuja au la?

Baada ya muda mfupi akajitokeza mmoja kati ya wafuasi wa UVCCM, na kutangaza kuwa, kikao hicho kimeghairishwa hadi hapokitakapopangwa tena.

“Jamani samahanini kwa usumbufu uliojitokeza, tumepata taarifa kwamba Mheshimiwa hatakuja leo amepata dharula hivyo kikao hakipo, hadi tutakapo wapigia simu tena siku yoyote kuanzia kesho” alieleza mmoja kati ya wafuasi wake.

error: Content is protected !!