Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Jerry Silaa aingia mitini, kamati yataka Polisi wamkamate
Habari za Siasa

Jerry Silaa aingia mitini, kamati yataka Polisi wamkamate

Jerry Slaa, Mbunge wa Ukonga
Spread the love

 

KAMATI ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imeomba kibali kutoka kwa Spika Job Ndugai, cha kumkamata Mbunge wa Ukonga (CCM), Jerry Silaa, baada ya mbunge huyo kuingia mitini bila taarifa, alipotakiwa kuendelea kuhojiwa dhidi ya tuhuma zinazomkabili za kushusha heshima ya mhimili huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Ombi hilo limetolewa leo Alhamisi, tarehe 26 Agosti 2021 na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka, baada ya Silaa kutohudhuria kikao cha mahojiano, bila kutoa taarifa.

Kamati hiyo iliamua kuchukua hatua hiyo, baada ya Silaa aliyetakiwa kufika katika Ukumbi wa Bunge, jijini Dodoma, majira ya saa 5.00 asubuhi, kutotokea.

“Leo tulikuwa na shauri, tulikuwa tunaendelea na mashauri yetu ambayo yako kwenye kamati. Tunaendelea na shauri la Jerry Silaa, ambaye yeye hakufika mbele ya kamati hii na hatuna taarifa naye. Hatukupata taarifa yoyote ya kwa nini hatofika kwenye kamati,” amesema Mwakasaka.

Mwakasaka amesema “kwa mujibu wa kanuni na sheria ambazo ni za haki, kinga, maadili na madaraka ya Bunge, spika yeye ni mleta shauri. Tulichofanya kwa kutumia sheria hizo hizo, nimeomba kibali kwa spika ili aweze kukamatwa na kuletwa hapa kama ambavyo sheria inaturuhusu.”

Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Maadili ya Bunge, amesema Spika Ndugai akiridhia ombi hilo, Silaa anatakiwa afikishwe mbele ya kamati hiyo kesho majira ya saa 4.00 asubuhi.

“Sababu hakuleta taarifa yoyote, hata mahakama ya kawaida usipoleta taarifa siku ya kufika mahakama huwa inaandiliwa arrest warrant, sisi kamati tumeomba kwa Spika ikiwezekana kesho saa nne aletwe hapa,” amesema Mwakasaka.

Mwakasaka amesema shauri hilo linaendelea kama kawaida “shauri linaendelea sababu juzi tulikuwa hatujamaliza, anaendelea na kiapo chake kile kile na ana taarifa za kutosha lakini tulimsubiri muda wa kutosha hakuleta taarifa yoyote.”

3 Comments

  • Yani sisiemu ni vilaza wa hali ya juu,, Yan kila kitu polisi,, Je kama aliugua ghafla atakujaje?? Kwan polisi wamekuwa nani Tanzania wa kutumiwatumiwa hovyo,, Hata siku hizi polisi wako kwa ajili yenu mnawatumia kama mnavyotaka ,, Jeshi la polisi pia lazma wawe na Msimamo, wafanye kazi kulingana na taratibu na Sheria kama ilivyo elekezwa,,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

error: Content is protected !!