January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jenister ataka wafanyakazi wote wawe na mikataba

Spread the love

WAZIRI wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenister Mhagama leo¬†ametembelea ofisi za kazi mkoani hapa ili kuona utendaji wa ofisi hiyo. Anandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Katika ziara hiyo Mhagama aliitaka ofisi ya kazi kuhakikisha inasimamia usawa kazini ikiwa ni pamoja na watumishi kupatiwa mikataba sahihi.

Akizungumza na wafanyakazi pamoja na viongozi wa vyama vya wafanyakazi mkoa wa Dodoma, amesema ni wajibu wao wa kuhakikisha wanasimamia maagizo ambayo yanasimamiwa na serikali kupitia Wizara husika.

Amesema mbali na mambo mengine amewataka idara ya wafanyakazi wanatakiwa kuzingatia sheria za kazi ikiwa ni pamoja na kukata makato sahihi kwa ajili ya mifuko ya jamii.

Waziri huyo amesema katika kufanya kazi katika mazingira rafiki na wafanyakazi wahakikishe haki na usawa unatendeka kwa kila mtumishi na asiwepo mtu wa kujifanya miungu watu.

“Sasa natoa agizo kila mahali pa kazi ni lazima kuwepo na chama cha wafanyakazi na haki inatakiwa kutendeka bila kuwepo kwa ubabaishaji.

“Pia watumishi wageni wote wanatakiwa kupewa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha wanajenga mahusiano mazuri na wafanyakazi wengine na pasiwepo na vikwazo vyovyote,” amesema Mhagama.

Muhagama pia alitaka taasisi mbalimbali kama OSHA, CMA, TUCTA, TUGHE na RAAWU kuhakikisha wanatimiza majukumu yao huku wakishirikishwa katika vikao mbalimbali vya maamuzi.

Katika kikao hicho Muhagama aliwataka viongozi wa idara ya kazi kuhakikisha wanafuatiria katika maeneo yote ya kazi ili kutambua wafanyakazi wote kama wana mikataba au la.

“Wapo wafanyakazi wengi katika nyumba za kulala wageni, mahoteli na maeneo mbalimbali ambao wanafanyakazi bila kuwa na mikataba jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.

“Umefika wakati wa kutoa mikataba ya watumishi wote kuhakikisha wanapatiwa mikataba ya uhakika na kupelekwa makato sahihi katika mifuko ya bima ya kijamii,” amesema.

Mbali na hilo alifanya ziara katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Dodoma Canivel ambako alibaini kuwa wapo wafanyakazi wengi ambao wanafanyishwa kazi kama sehemu ya mazoezi wakati hawana mikataba yoyote ya uhakika.

error: Content is protected !!