June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jengo la Posta Dodoma lateketea kwa moto

Spread the love

JENGO Posta lililopo katika eneo la sabasaba katika Manispaa ya Dodoma limeteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa, anaandika Dany Tibason, Dodoma.

Akizungumzia kutekeleza kwa jengo hilo Meneja wa Posta Mkoa wa Dodoma, Magreth Mlyomi amesema mpaka sasa kuna hasara kubwa kutokana na kutekeleza jengo hilo sambamba na vifaa vyote vya ofisi.

Mlyomi amesema licha ya kuwa hakuna mfanyakazi hata mmoja aliyepoteza maisha katika jengo hilo lakini mpaka sasa kuna vitendea kazi vingi vya ofisi pamoja na mizigo ya wateja.

“Kuna mizigo mingi pamoja na vifaa vya kazi vyote vimeteketezwa na moto na kwa taarifa nilizopata kulikuwa na mizigo ya watu ,niliambiwa kuwa moto umeanza majira ya saa nne asubuhi na inaonesha kuwa chanzo cha moto ni umeme,” ameeleza Meneja.

Akizungumzia kuhusu masuala ya miundombinu ya maeneo husika amesema ni mibovu na kutokana na changamoto hiyo suala hilo lipo katika mamlaka husika ya manispaa.

Kwa upande wake katibu wa wafanyabiashara katika soko la Sabasaba katika Manispaa ya Dodoma, Gergod Lugusi amesema majira ya saa nne asubuhi kulitokea moto mkali ambao uliunguza jengo hilo.

Amesema chanzo cha moto huo inasemakana kuwa ni tatizo la umeme na uongozi ulilazimika kutoa taarifa katika kikosi cha zima moto na bila kuchelewa walifika kwa wakati.

Hata hivyo amesema licha ya kufika kwa wakati katika tukio bado kikosi hicho kilikutana na kikwazo kwa kutokana na miundombinu kuwa mibovu na migumu kupitika.

error: Content is protected !!