February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Jenerali Waitara kuongoza uchunguzi ajali MV Nyerere

Spread the love

JENERALI Mstaafu, George Waitara kuongoza jopo la wajumbe saba wa Tume ya kuchunguza ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea tarehe 20 Septemba mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Tume hiyo imetangazwa leo tarehe 24 Septemba 2018 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akitaja majina ya wajumbe wa tume hiyo katika kijiji cha Bwisya kisiwani Ukara wilaya ya Ukerewe, Mwanza.

Waziri Majaliwa amesema wajumbe hao wanatakiwa kukamilisha uchunguzi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.

Wajumbe waliotangazwa na Waziri Majaliwa ni pamoja na Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi, Mhandisi Marcelina Magesa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Queen Mlozi, Wakili Julius Kalolo.

Wengine ni SACP Camillus Wambura na Mkurugenzi wa Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu Hussein.

Hadi sasa jumla ya watu 41 wameokolewa na wengine 227 wamepoteza maisha baada ya miili mingine mitatu kupatikana leo asubuhi.

error: Content is protected !!