October 23, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Jenerali atishia vita Burundi

Sehemu ya wakimbizi wa Burundi walioingia Tanzania

Spread the love

BURUNDI imo hatarini kuingia kwenye vita baada ya Jenerali aliyeshirikijaribio la kumpindua Rais Pierre Nkurunziza kutishia kuanzisha mapambano ya kumng’oa madarakani.

Jenerali Leonard Ngendakumana, aliyekuwa msaidizi wa kiongozi wa mapinduzi yaliyoshindwa Aprili mwaka huu, amemshutumu Nkurunziza kwa kuzorotesha usalama wa nchi hii mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, na kuihatarisha kutumbukia katika vita vya wenyewewe.

“Hatua iliyobaki ni kujipanga kwa ajili ya kumdhibiti, kumsukuma Pierre Nkurunziza afahamu kuwa anapaswa kwa hiari yake kung’atuka madarakani si hivyo ajiandae tumtoe kwa nguvu, kwa kuanzisha mapambano ya kijeshi,” amesema Jenerali Ngendakumana akinukuliwa na televisheni ya KTN ya Kenya.

Jenerali Ngendakumana amesema Jenerali Godefroid Niyombare aliyeongoza mapinduzi yaliyoshindwa, angali ndani ya Burundi.

Tamko la jenerali huyo limepokewa kwa kauli kali ambapo serikali imelijibu tamko hilo kwa kusema hatua yoyote ya mapambano itajibiwa kwa mapambano.

“Mtu yeyote yule anayetishia usalama wa Burundi, akitokea ndani au nje ya nchi, atakabiliana na nguvu ya jeshi na vikosi vyetu vya usalama,” amesema Gervais Abayeho, Msemaji wa Rais Nkurunziza.

Ngendakumanaamesema serikali ya Burundi inakusudia kuingiza kanda hii kwenye vita vya kikabila.

Mahojiano na Jenerali Ngendakumana yalifanywa katika eneo ambalo halikutajwa ikiwa ni kwenye mkesha wa mkutano wa viongozi wakuu wa Afrika Mashariki pamoja na Afrika Kusini kuhusu kutafuta ufumbuzi wa mgogoro unaohusu uamuzi wa Nkurunziza kuamua kugombea tena urais baada ya vipindi viwili vya uongozi.

Wakuu wa Afrika Mashariki wametaka serikali ya Burundi iahirishe uchaguzi mkuu wa rais kwa wiki mbili kutoka Julai 15 ulipopangwa ufanyike ili kuruhusu majadiliano ya vikundi vinavyovutana.

Awali serikali ilikataa shinikizo za kuahirisha uchaguzi unaotarajiwa ikiwa ni siku chache tangu ufanyike uchaguzi wa bunge uliosusiwa na vyama vya upinzani.

Wapinzani wa Rais Nkurunziza wanasema kitendo cha kugombea kwa mara ya tatu kilichokuwa chimbuko la mgogoro kwa kuanza ghasia kumshinikiza afute azma yake, na kusababisha mapambano kati ya waandamanaji na polisi kwenye mji mkuu Bujumbura.

Rais Nkurunziza amekuwa akisisitiza kuwa Mahakama imetoa uamuzi wa kumruhusu kugombea tena.

Pamoja na kutaka uchaguzi uahirishwe kwa sasa, viongozi wa Afrika wamemteua Rais Yoweri Museveni wa Uganda kuanzisha majadiliano.

Mkataba wa amani wa uliofikiwa jijini Arusha mwaka 2010, ambao ulimaliza vita vya miaka 12 kati ya kundi la waasi wa Kihutu likiwemo linaloongozwa na Nkurunziza mwenyewe dhidi ya Watutsi, uliunganisha jeshi la taifa.

Kwa sasa jeshi na taasisi nyingine za kiutawala zimegawanyika.

Jenerali Ngendakumana amesema waliounga mkono mapinduzi ndio wanaotupa mabomu ya mkono, yakilenga vituo vya polisi hadi wakati wa uchaguzi wa bunge uliofanyika Juni 26.

“Tunawaunga mkono, na nia yetu ni kuongeza mashambulizi,” anasema.

Watamazaji wa UN wamesema uchaguzi huo haukuwa huru wala wa haki, uamuzi ambao serikali imeupinga.

Chanzo Aljazeera.

error: Content is protected !!