August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jela kwa ujangili wa meno ya tembo

Nyundo ya Hakimu

Spread the love

MAHAKAMA ya Wilaya ya Manyoni, imewahukumu kifungo cha miaka 25 jela kila mmoja majangili wawili baada ya kutiwa hatiani kwa makosa mbalimbali ikiwemo kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya Sh. milioni 31.5, anaandika Mwandishi Wetu.

Washtakiwa hao ni George Mhando na Magawa Chikole. Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Singida, Joyce Minde baada ya kusikiliza ushahidi kutoka upande wa mashtaka ambao uliwasilisha mashahidi wa tano.

Amesema washtakiwa hao wametiwa hatiani kwa kukutwa na meno ya tembo, kujihusisa na mtandao wa biashara ya nyara za serikali.

Akisoma hukumu hiyo, alisema kufuatia kukutwa na makosa hayo washtakiwa hao wamehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela kila mmoja au kulipa faini ya Sh. milioni 315.

Wakati huo huo, washtakiwa watatu wa makosa ya ujangili wa meno ya tembo yenye thamani ya Sh. milioni 31.5 wamehukumiwa kifungo cha miaka saba kila mmoja.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Manyoni, Ferdinand Kiwonde, akisoma hukumu hiyo, alitaja washtakiwa hao kuwa niMasado Maile (39), Emmanuel Mwaluko (36), Mazengo Charahani (52), wakazi wa Bahi na Chibago Muwinje (60) na Masimba Chingole (36), wakazi wa Manyoni.

Amesema katika kesi hiyo washtakiwa watatu wamekutwa na kosa la kukutwa na meno ya tembo na kujihusisha na mtandao wa nyara za serikali.

error: Content is protected !!