Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Jecha ‘Hasimu’ wa Maalim Seif,  ajitosa mbio za urais Zanzibar
Habari za Siasa

Jecha ‘Hasimu’ wa Maalim Seif,  ajitosa mbio za urais Zanzibar

Spread the love

JECHA Salum Jecha, aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), amechukua fomu ya kugombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Jecha amechukua fomu hiyo leo Jumamosi tarehe 20 Juni 2020 katika Ofisi Kuu ya CCM Zanzibar, iliyoko Kisiwandui.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, Jecha amesema endapo atafanikiwa kuteuliwa na CCM kugombea urais kisha kuchaguliwa na wananchi kushika nafasi hiyo, atawaunganisha wananchi wa Zanzibar.

“Madhumuni yangu makubwa kama nitapata ridhaa ya CCM, ikinipendekeza kugombea ni kuwaunganisha wananchi wa Zanzibar na Watanzania kwa ujumla, katika shughuli za kimaendeleo, kijamii na nyinginezo, “ amesema Jecha na kuongeza:

“Nitajitahidi ili nisimamie haki za watu wote bila kubagua dini, itikadi za kisiasa, wala mtu anatoka wapi. Watu wote kwangu ni sawa, nitaenzi yote yaliyoanzishwa tangu mapinduzi mpaka leo wala sitabagua .”

Jecha aliyekuwa mwenyekiti wa ZEC kuanzia mwaka 2015 hadi 2018, ameweka historia kubwa katika harakati za Maalim Seif Shariff Hamad, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, za kugombea Urais wa Zanzibar, kufuatia hatua yake ya kufuta matokeo ya Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015.

Mwenyekiti huyo mstaafu wa ZEC, wakati alipokuwa madarakani, alifuta matokeo ya uchaguzi huo, kwa maelezo kwamba ulikuwa na dosari nyingi, kufuatia ukiukwaji wa sheria za uchaguzi.

Jecha alitaja ukiukwaji huo kuwa ni, idadi kubwa ya wapiga kura ikilinganishwa na idadi halisi ya watu waliojiandikisha katika  baadhi ya vituo, pamoja na vyama vya siasa kuingilia majukumu ya ZEC, kwa kujitangazia ushindi.

Jecha alitangaza kuufuta uchaguzi huo , siku moja baada ya Maalim Seif, aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF), kujitangaza kwamba ni mshindi wa uchaguzi huo, uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2020.

Baada ya kuufuta matokeo ya uchaguzi wa rais, Jecha aliitisha tena uchaguzi huo mwezi Machi 2016, lakini CUF kilisusa kushiriki uchaguzi huo, kwa madai kwamba haukuwa halali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!