September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

January amshukuru Rais Samia, aahidi kupiga kazi kivitedo

Spread the love

 

JANUARY Makamba, Waziri wa Nishati nchini Tanzania, ametoa shukrani kwa wote waliompongeza kwa kuteuliwa kuwa waziri na kuwaahidi kuwatumikia kwa vitendo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Makamba ambaye ni Mbunge wa Bumbuli (CCM), ametoa pongezi hizo baada ya juzi Jumatatu, tarehe 13 Septemba 2021, Ikulu ya Chamwino Dodoma, kuapishwa kuwa waziri wa nishati.

Amechukua nafasi ya Dk. Merdard Kalemani, Mbunge wa Chato ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Makamba aliyewahi kuwa Waziri wa Muungano na Mazingira ameandika “nawashukuru nyote mlionitumia ujumbe wa pongezi na kunitakia heri. Sio kazi nyepesi lakini nitajitahidi.”

“Namshukuru Mhe Rais @SuluhuSamia kwa imani aliyoionyesha kwangu. Sitamuangusha. Katika wiki zijazo, tutaonyesha kwa vitendo umuhimu wa sekta hii kwa mustakabali wa nchi.”

Mbali na kuwa waziri wa Muungano na Mawasiliano, Makamba amewahi kuwa naibu waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia.

error: Content is protected !!