October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Janga la Corona: Mbowe ampa mtihani Rais Magufuli

Spread the love

FREEMAN Mbowe, Kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amemhoji Rais John Magufuli ya kwamba, idadi ngapi ya vifo vitakavyotokana na Ugonjwa Homa Kali inayosababishwa na Virusi vya Corona (COVID-19), itamfanya achukue hatua madhubuti za kuudhibiti. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mbowe amehoji hayo leo tarehe 11 Aprili 2020 katika ukurasa wake wa Twitter, siku moja baada ya Rais Magufuli kuweka bayana kwamba, serikali yake haiko tayari kufungia watu ndani na mipaka ya nchi, kwa kuwa hatua hiyo inaweza leta madhara kwa taifa, hasa anguko la uchumi.

“Ulimwengu unalia na kuomboleza kutokana na maisha ya watu kupotea, uchumi wa dunia unaanguka kwa kasi isiyo ya kawaida. Ni idadi gani ya watu watakaopoteza maisha, itakayokufanya uone huu ugonjwa ni janga?” amehoji Mbowe.

Mbowe ameeleza kuwa, uchumi wa nchi unaweza kuimarishwa pindi utakapoyumba, lakini maisha ya watu yatakayopotea kutokana na ugonjwa wa COVID-19, hayawezi rejeshwa.

“Hotuba ya rais kuhusu janga la Corona katika ibada ya Ijumaa Kuu nyumbani kwao Chato inatia huruma. Hakuna kufungia watu ndani kwa sababu anataka kuokoa uchumi na miradi yake ya miundombinu. Maisha ya watu wetu hatuwezi kuyarudisha lakini kwa uchumi tunaweza,” ameandika Mbowe.

Kwa mujibu wa wizara ya afya, Tanzania ilikuwa na wagonjwa 32 wa COVID-19, ambapo watano kati yao wamepona huku watatu wakifariki dunia.

error: Content is protected !!