Monday , 5 June 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Jammeh sasa ahesabiwa dakika
Kimataifa

Jammeh sasa ahesabiwa dakika

Yahya Jammeh, Rais wa Gambia aliyeangushwa katika uchaguzi Mkuu
Spread the love

MUDA wa kubembelezwa kwa Yahya Jammeh Rais wa Gambia aliyegoma kuondoka Ikulu ya nchi hiyo baada ya kuangushwa na mpinzani wake Adama Barrow sasa umekwishwa rasmi na muda wowote ataondolewa kwa nguvu, anaandika Wolfram Mwalongo.

Jeshi la Jumuiya ya Afrika Magharibi (ECOWAS) lipo tayari kupambana na Rais Jammeh ambapo kwa muwamjibu wa shirika la habari la Aljazeera kiongozi huyo aliongezewa muda kutoka jana hadi leo mchana.

Tayari majeshi ya ECOWAS yametua kwenye ardhi ya Gambia na kinachosubiriwa ni amri ya kuanza kwa mapambano ya kumtoa Jammeh Ikulu. Tayari wasaidizi muhimu wa rais huyo wameshamkacha na kujiweka kando na mkakati wake wa kung’ang’ania madaraka.

Edward Anthony  Mwanasheria aliyekubali kumsimamia kesi yake kwenye Mahakama Kuu ya nchi hiyo kupinga matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana sasa yupo uhamishoni.

Anthony alimwandikia barua mteja wake (Rais Jammeh) na kumsihi akabidhi madaraka kwa amani kwa aliyekuwa mpinzani wake Adama Barrow aliyetangazwa kushinda uchaguzi huo.

Tayari Rais Barrow ameapishwa rasmi kuwa rais wa taifa hilo ingawa hafla ya kuapishwa kwake imefanyika nchini Senegal ndani ya ubalozi wa Gambia.

Aidha, Jeshi la Gambia limesema lipotayari kumuunga mkono Rais Adama Barrow ambaye aliapishwa jana nchini Senegal.

Hata hivyo (ECOWAS) imesema Rais Jammeh hatakiwi kuendelea kubaki kwenye ardhi ya Gmabia kutokana na kuhofia usalama wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Miili ya waliofariki kwenye ajali ya treni India, kukabidhiwa baada ya vipimo vya DNA

Spread the love  TAKRIBANI watu 260 wamefariki na wengine karibu 650 wamejeruhiwa...

Kimataifa

Kauli ya Rais wa China kuhusu ajira yawakatisha tamaa vijana

Spread the love  KAULI ya hivi karibuni ya Rais wa China, Xi...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Jeshi la Sudan lasitisha mazungumzo na wanamgambo wa RSF

Spread the love  JESHI rasmi la serikali ya Sudan, limesitisha ushiriki wake...

Kimataifa

Wakimbizi laki mbili wa Kongo, Burundi kuhemea chakula

Spread the love  SHIRIKA la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP), limetangaza...

error: Content is protected !!