August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jammeh akomba fedha, atokomea Guinea

Yahya Jammeh, Rais wa Gambia aliyemaliza muda wake, akishuka kwenye ndege

Spread the love

YAYHA Jammeh aliyekuwa rais wa Gambia ameliacha taifa hilo kwenye machungu, baada ya kukomba fedha katika hazina na kwenda uhamishoni nchini Guinea ya Ikweta, anaandika Wolfram Mwalongo.

Mapema baada ya kutangaza kupitia Televisheni ya taifa hilo kwamba ataondoka Ikulu ya nchi hiyo, hatimaye ameondoka na kuchota Dola ya Kimarekani 11 milioni.

Shirikika la habari la Aljazeera limeripoti kwamba wizi huo wa fedha umefanywa siku chache kabla ya kung’oka Ikulu, baada ya kushauriwa na marais Mohamed Abdel Aziz wa Mauritania na Alpha Conde wa Guinea ya Ikweta.

Mia Ahmad Fatty Mshauri maalumu wa Rais Adama Barrow amewaambia waandishi wa habari nchini Senegal kwamba tathimini ya kiasi kilicho baki na kilichotoka inaendelea kufanyika.

Aidha, amesema hali ya uchumi wa Gambia imendelea kuzorota siku za hivi karibuni hali inayotishia kukumbwa na mdororo wa uchumi katika siku zijazo.

Kwa sasa katika mji wa Banjul wafuasi wa Rais Barrow wamejitokeza kwenye mitaa mbalimbali wakifurahia maandalizi ya ujio wa rais wao aliyeapishwa uhamishoni nchini Senegal.

Aidha vikosi vya jeshi la Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), vimendelea kuimarisha ulinzi Ikulu ya nchi hiyo kwa ajili ya mapokezi ya rais huyo aliye uhamishoni nchini Senegal.

Barrow aliapishwa tarehe 19 Januari katika viwanja vya ubalozi wa Gambia nchini Senegal. Hatua hiyo ilikuja kutokana na sintofahamu iliyogubika taifa hilo haswa rais mstaafu Jammeh kutangaza wazi kwamba hang’oki madarakani.

error: Content is protected !!