July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jamii yasisitizwa kudhibiti maambukizi ya kipundupindu

Spread the love

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa rai kwa jamii, wataalamu wa afya na viongozi katika ngazi zote kutimiza wajibu wake katika harakati za kuudhibiti ugonjwa wa Kipindupindu. Anaandika Regina Mkonde … (endelea).

Pia, mikoa imetakiwa kutuma taarifa sahihi zinazohusu mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu na kuwachukulia hatua kali watumishi watakao zembea au kujaribu kuficha taarifa hizo.

Hatua hii imefikiwa na wizara baada ya ongezeko la idadi ya wagonjwa badala ya kupungua. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Wizara hiyo Ummy Mwalimu, imesema kuwa kwa kipindi cha wiki iliyopita(tarehe 11-17) jumla ya wagonjwa wapya ilikuwa 549 na vifo 10.

Idadi hiyo ya wagonjwa wapya imefikisha idadi ya watu 14,105 waliougua kipindupindu na vifo 218 tangu ugonjwa huo ulipuke. Vilevile idadi ya mikoa ambayo imeripoti wagonjwa wapya imeongezeka kutoka mikoa 11 hadi 16 ukilinganisha na wiki iliyopita.

“Karibia mikoa yote ya Tanzania Bara ilikwisha athirika na ugonjwa huu isipokuwa Njombe,Ruvuma, na Mtwara ambayo haijwahai kuripoti mgonjwa yeyote wa kipindupindu.” Alisema Ummy

“Mikoa iliyorudia kuripoti wagonjwa wapya baada ya kuudhibiti kwa wiki zilizopita ni Dar Es Salaam, Lindi, Rukwa, Kagera na Kilimanjaro. Mikoa ambayo imeendelea kuripoti wagonjwa ni pamoja na Morogoro, Arusha, Singida, Manyara, Pwani, Dodoma, Geita, Mara, Mwanza na Simiyu.” Aliongeza

Ummy alidai kuwa, Kati ya mikoa hiyo mkoa wa Morogoro umeendelea kuwa kinara wa kuripoti idadi kubwa ya wagonjwa(Manispaa ya Morogoro 120, Halmashauri 40) ukifuatiwa na Simiyu(Bariadi 50), Manyara (Simanjiro 41) Mwanza (Ukerewe 24 na Halmashauri ya Arusha)

Wizara imeendelea kuikumbusha jamii kuwa kipindupindu ni ugonjwa unaoambukizwa kwa kula chakula au kinywaji chenye vimelea ambavyo hupatikana kwenye kinyesi na matapishi ya mgonjwa wa kipindupinduau kwenye kitu chochote kilichochafuliwa na kinyesi au matapishi ya mgonjwa.

Wananchi wanasisitizwa kuzingatia unywaji wa maji yaliyo safi na salama, kuepuka kula chakula kilichoandaliwa katika mazingira yasiyo safi na salama, kunawa mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka, kutumia vyoo wakati wote na kutojisaidia ovyo katika vyanzo vya maji vya mito, maziwa na mabwawa.

Ummy alimaliza kwa kutoas agizo kwea Mamlaka za Mikoa na Halmashauri pamoja na watendaji wake kote nchini kuendeleza juhudi za kuzuia kusambaa kwa mlipuko ambazo ni ushiriukishwajiwa viongozi ngazi mbalimbali hasa ngazi za Halmashauri kwa kushirikiana na madiwani na viongozi wa kata, vijiji na mitaa.

Mamlaka husika kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama ikiwa ni pamoja na uwekaji wa dawa ya klorini kwenye maji na kupima usalama wa maji mara kwa mara. Upatikanaji wa dawa za kutibu maji(Water Guard, Aqua Tabs) katika maeneo ya mlipuko.

error: Content is protected !!