Saturday , 2 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Jamhuri yakwamisha kesi ya Chadema dhidi ya Jeshi la Polisi
Habari za SiasaTangulizi

Jamhuri yakwamisha kesi ya Chadema dhidi ya Jeshi la Polisi

Spread the love

 

MAHAKAMA Kuu, Masjala ya Dodoma, imeahirisha usikilizwaji wa kesi ya Chadema dhidi ya Jeshi la Polisi baada ya Mawakili wa Jamhuri kutofika Mahakamani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Chadema, ilifungua shauri hilo jana kuiomba Mahakama itoe amri kwa Jeshi la Polisi kumfikisha mahakamani au kumuacha kwa dhamana Mratibu wa Uhamasishaji wa Baraza la Vijana (Bavicha), Twaha Mwaipaya.

Kesi hiyo iliyopo mbele ya Jaji Adam Mambi imeahirishwa leo Jumanne, tarehe 5 Julai 2022, hadi Jumatatu ijayo ya tarehe 11 Julai 2022.

Wakili wa Mwaipaya, Fred Kalonga amedai baada ya upande wa Jamhuri kutotokea mahakamani kwa ajili ya usikilizwaji wa maombi hayo, licha ya kupewa wito wa mahakama, walimuomba Jaji Mambo kesi iahirishwe hadi kesho, lakini alikataa ombi hilo akisema atakuwa safarini.

Wakili huyo amedai, mteja wake anayeshikiliwa na Polisi tangu akamatwe tarehe 30 Juni 2022, hakufikishwa mahakamani hapo.

“Maombi yalipangwa mbele ya Jaji Mambo, tumewapeleka wito wa mahakama jamhuri kwa maana ya IGP, RPC na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, lakini hakukuwa na upande wowote waliokuja mahakamani. Ikawa busara ya jaji kutoendelea na maombi hayo sababu upande mmoja haupo,” amedai Wakili Kalonga na kuongeza:

“Tukamuomba tuahirishe hadi kesho akatuambia anakwenda safari na tarehe atakayokuwepo ni Jumatatu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Mwalimu jela miaka mitatu kwa rushwa

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi, wilaya ya Igunga, mkoani Tabora imemhukumu...

Habari za Siasa

Rais Samia kuzindua programu ya nishati safi ya kupikia kwa wanawake Afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua programu ya...

Habari za Siasa

AG aiagiza kamati ya maadili kuwashughulikia mawakili wanaokiuka maadili

Spread the loveMWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Eliezer Feleshi, ameagiza Kamati...

Habari za Siasa

Jaji avunja ukimya sakata la Mpoki kusimamishwa uwakili

Spread the loveJAJI Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, amekitaka Chama cha...

error: Content is protected !!