Saturday , 3 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Jaji Warioba: Lazima tuwe na msimamo
Habari za Siasa

Jaji Warioba: Lazima tuwe na msimamo

Joseph Warioba, Waziri Mkuu Mstaafu
Spread the love

JAJI Joseph Warioba, Waziri Mkuu Mstaafu amezitaka nchi za Afrika kuwa na msimamo dhidi ya ukoloni mamboleo. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 25 Oktoba 2019, wakati akichangia hoja katika kongamano maalum la Vikwazo vya Kiichumi na Hatma ya Maendeleo ya Afrika, lililofanyika kwenye ukumbi wa Nkurumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

“Imefika wakati lazima tuwe na msimamo, kama tulivyopigania uhuru, huu mfumo mpya wa ukoloni mamboleo, tupaze sauti uondolewe,” amesema Jaji Warioba.

Wakati huo huo, Jaji Warioba ameitaka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kupaza sauti ili nchi za Afrika zisiweke vikwazo vya kiuchumi na Jumuiya za Kimataifa.

“Wanatia vikwazo na si kwa nchi moja tu, hata nchi isisyo na vikwazo ikisaidia nyingine, hiyo nchi inawekewekea vikwazo. SADC ipige kelele, ili nchi zisiwekewe vikwazo,” amesema Mzee Warioba.

“Mimi nilivyoliona hili tamko, naona tunaliwasha upya. Hili wazo lisiishie SADC,  lisonge mbele kuondoa vikwazo, na si vikwazo pekee lazima tuangalie kwa nini sasa hivi kuna mtindo wa kuweka vikwazo, ndipo tujadiliane.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!