Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Jaji Warioba akemea ubaguzi wa kivyama, ataka amani isiingiliwe 
Habari za SiasaTangulizi

Jaji Warioba akemea ubaguzi wa kivyama, ataka amani isiingiliwe 

Joseph Warioba, Waziri Mkuu Mstaafu
Spread the love

 

MWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Jaji Joseph Sinde Warioba, amekemea watu wanaotaka kuleta ubaguzi katika ukabila, udini, ukanda na uvyama, akisema wanahatarisha amani na umoja wa nchi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Jaji Warioba ametoa kauli hiyo leo Jumanne, tarehe 12 Oktoba 2021, kwenye Kongamano la Kumbukizi ya Miaka 22 ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere, kwenye Chuo  cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, jijini Dar ea Salaam.

Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Tanzania, amewaomba Watanzania wawe kitu kimoja, ili kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa jitihada zake za kuliunganisha Taifa.

“Mwalimu Nyerere alionya alipozungumza na wanahabari Machi 1995 Kilimanjaro, alizungunza mambo ambayo yanavunja umoja wetu na amani yetu. Nadhani ni wajibu wetu kama Watanzania,  viongozi na wananchi wa Tanzania tukemee watu wote ambao wanataka kuleta mambo ya ukabila,  udini, ukanda na mambo ya vyama. Watanzania tuwe kitu kimoja,” amesema  Jaji  Warioba.

Julius Nyerere, Hayati Baba wa Taifa

Jaji Warioba alitoa wito huo alipozungumzia kauli ya Rais Samia akiwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni, jijini Dodoma, akisema hatengui uteuzi wa watumishi wa umma kwa sababu za ukabila.

“Juzi nilimuangalia rais, nadhani hata jana akizungunzia mambo haya ambayo kwa msingi wa kujenga   mshikamano na amani yetu yanaanza kuchezewa,  yeye wanaanza kumlaumu kwamba akichukua hatua kwa watumishi wa umma wanaanza kusema kwa sababu ya ukabila, lakini ukweli kwa sasa hivi ukabila unaanza, udini unaaza kuzungumzwa sana, ukanda unaanza kuzungumzwa sana na uvyama unaanza kuzungumzwa, ile misingi iliyojenga umoja na amani katika nchi hii mnaanza kuingilia,” amesema Jaji Warioba.

Jaji Warioba amesema, Watanzania wanapaswa kuilinda amani kwa kuwa haikuja hivi hivi bali kuna misingi ilijengwa.

“Amani ilijengwa haikuja hivi hivi ilijengwa,  Mwalimu Nyerere wakati anapigania uhuru aliamua na akawa waziwazi kujenga taifa lenye umoja, lenye amani na ndiyo kazi ya kwanza aliyoyafanya. Siku hizi tunazungumzia haya mambo tunaona kama kitu rahisi, haikuwa rahisi ilikuwa kazi ngumu,” amesema Jaji Warioba.

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini Tanzania, amesema Mwalimu Nyerere alitokea katika familia ya kichifu, lakini alivunja desturi hiyo kwa ajili ya kuondoa ubaguzi.

“Mwalimu Nyerere alikuwa mtoto wa chifu na kaka yake aliyemlea alikuwa chifu, lakini alisema tuvunje uchifu. Mtoto wa chifu anavunja uchifu haikuwa kazi rahisi, kuanzia nyumbani kwake watu hawakupenda kuondoa uchifu lakini alifanya hivyo,” amesema Jaji Warioba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Jaji Biswalo aendelea kung’ang’aniwa fedha za ‘Plea Bargaining’, CUF wataka ajiuzulu

Spread the love  CHAMA cha Wananchi (CUF), kimemtaka aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka...

Habari za Siasa

Bunge labaini madudu mfumo ukusanyaji mapato, h’shauri tatu kikaangoni

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali...

Habari za Siasa

Mkuu wa wilaya ya Rungwe azindua vyumba sita vya madarasa vya thamani ya 64 mil

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu amezindua vyumba...

Habari za Siasa

Mbunge afurahia mabilioni ya Samia kutua jimboni

Spread the love  MBUNGE wa Igunga, Nicholas Ngassa ameishukuru Serikali kwa utekelezaji...

error: Content is protected !!