September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jaji Warioba aingia hofu

Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba

Spread the love

JAJI Mstaafu, Joseph Sinde Warioba ameingiwa na hofu kutoa maoni yake kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa, uliofanyika tarehe 24 Novemba 2019. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Uchaguzi huo, ulisuswa na vyama vya upinzani vyenye nguvu nchini, kwa madai ya kuchafuliwa na wasimamizi wake.

Alipoulizwa maoni yake kuhusu uchaguzi huo, Jaji Warioba alijibu sina maoni.

Hata hivyo, mwandishi aliendelea kumdadisi, na kisha kumchomekea tena kuhusu fikra zaje juu ya uchaguzi huo.

Haraka Jaji Warioba alitoa jibu lilelile no comment.

Vyama vinane vilivyosusa kushiriki uchaguzi huo ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF), ACT- Wazalendo, Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), UPDP na NCCR-Mageuzi.

Tarehe 25 Novemba 2019, Seleman Jafo, Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI alitangaza matokeo ya uchaguzi huo, na kwamba CCM kimepata wenyeviti wa vijiji 12,260 kati ya 12,262, pamoja na mitaa yote 4,263 sawa na asilimia 100.

Pia, kimepata wenyeviti wa vitongoji 63970 kati ya 63992, wajumbe kundi la wanawake 106,577 kati ya 106,622 na wenyeviti mchanganyiko 144,925 kati ya 145,021.

error: Content is protected !!