Monday , 30 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Jaji Siyani aapishwa, akabidhiwa majukumu
Habari za Siasa

Jaji Siyani aapishwa, akabidhiwa majukumu

Spread the love

 

JAJI Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mustapha Siyani, amekabidhiwa rasmi majukumu yake mapya baada ya kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan, leo Jumatatu, tarehe 11 Oktoba 2021, kwenye Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mbali na Jaji Siyani, viongozi wengine walioapishwa leo ni, Sophia Mjema, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Jaji Omar Othmani Makungu, kluwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania.

Jaji Siyani anayesimamia kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, katika Mahakama Kuu ya Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam, aliteuliwa na Rais Samia kushika wadhifa huo tarehe 8 Oktoba mwaka huu.

Akizungumza baada ya kumuapisha, Rais Samia amemuagiza Jaji Siyani aimarishe shughuli za mahakama kupitia njia ya mtandao pamoja na kusimamia.

“Nategemea mtakwenda kutenda haki kama mnavyotakiwa, Jaji Mkuu Kiongozi juzi tulipokuwa na shughuli ya kufungua vituo jumuishi vya kutoa haki, kuna mambo mengi niliagiza yakiwemo yale ya kuimarisha shughuli za mahakama kwenda mtandao. Naomba ukalisimamie vizuri,” amesema Rais Samia na kuongeza:

“Najua kuna upungufu wa bajeti, kwenye hili nikaomba waziri na wewe mkae muone jinsi ya kufanya. Mkishindwa tuone tunasukuma vipi, lakini kwa sasa hivi lazima twende na mitandao kutatua matatizo au mashauri yanayoletwa kwenye mahakama.”

Kwa upande wake Makamu wa Rais, Dk. Phillip Mpango, amewataka majaji walioapishwa leo, kuimarisha ushirkiano kati ya mhimili huo na mihimili mingine.

“Nakazia aliyosema Jaji Mkuu la kushirikiana kati ya mihimili, nimekuja kukumbana na kesi kama mbili hivi mahakama inaamua lakini hukumu haitekelewi. Kwa hiyo unakaa unasema kitu gani hiki,” amesema Dk. Mpango.

Makamu huyo wa Rais wa Tanzania, amewaagiza majaji na mahakimu nchini, wahakikishe hukumu wanazozitoa zinatekelezwa ili haki za wananchi zipatikane.

“Mahakimu waliangalie hili, sitarajii kwamba kazi inaishia hapa. Tunajua haki inatolewa juu kwa Mungu, lakini hapa duniani nyie ndio mnatoa haki,” amesema Dk. Mpango na kuongeza:

“Ni vizuri mkawa na namna ya kufuatilia hukumu zinazotolewa na mahakama kama zinatekelezwa au hapana ili vyombo vinavyohusika viweze kusimamia haki za wananchi wetu ambao wanaililia kila siku.”

Naye Jaji Mkuu wa Tanzania, amemuagiza Jaji Siyani asimamie nguzo tatu za Mahakama katika utekelezaji wa majukumu yake mapya.

“Naamini utasimamia zile nguzo zetu tatu zinazotuongoza kwenye mpango mkakati wetu, moja utawala bora, uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali. Pili, upatikanaji na utoaji haki kwa wakati. Tatu, kuimarisha imani ya wananchi sababu bila imani ya wananchi mahakama haina faida,” amesema Prof. Juma.

Prof. Juma amemtaka Jaji Siyani atumie busara katika utekelezaji wa majukumu yake, kuondoa matabaka katika taasisi za mahakama pamoja na kusimamia mkakati wa mhimili huo wa kuhamisha shughuli zake katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

“Unatakiwa uwe na busara, umri wako mdogo wewe kiongozi utaongoza watu wenye umri mkubwa zaidi yako. Busara, hekima na ubinadau ni jambo ambalo kiongozi yoyote katika nafasi yako anakuwa nayo. Lazima uelewe mahakama ikwenda wapi,” amesema Prof. Juma na kuongeza:

“Uelewe safari ya mahakama kwenda mtandao, hiyo ni dhahiri kwamba tumeshajiwekea vigezo. Tumefanya uwekezaji mkubwa katika TEHAMA, sasa ni wakati wa kufanya uwekezaji ule uwe na matunda, sasa wewe ni msimamizi muhimu sana katika hilo.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chongolo asikitishwa na mradi wa Mil 900 kutoanza kutoa manufaa

Spread the loveKATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya

Spread the love  MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Bara,...

error: Content is protected !!