October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jaji Mutunga wa Kenya azindua kitabu Tanzania

Jaji Mstaafu wa Kenya, Willy Mutunga (kulia) akizindua kitabu sambamba na Jaji Joseph Warioba na Jaji Mstaafu wa Tanzania, Othman Chande

Spread the love

 

JAJI Mkuu Mstaafu wa Kenya, Willy Mutunga amezindua kitabu chake alichokipa jina la ‘Beacons of Judiciary Transformation’ leo Ijumaa tarehe 29 Aprili 2022, jijini Dar es Salaam nchini Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Jaji Mutunga aliyehudumu kama Jaji Mkuu wa Kenya kwa miaka minne kuanzia 2010-2014, amezindua kitabu hicho chenye mchanganyiko wa hotuba zake, maamuzi yake na maandiko ya kitaalamu, kikiwa na kurasa 504.

Jaji huyo aliyeingia madarakani baada ya kuundwa kwa Katiba Mpya katika taifa hilo, amesema katika kitabu chake hicho ameandika hotuba zake 60, maamuzi saba ya kesi alizohukumu akiwa kama Jaji Mkuu na maandishi ya kitaalamu matatu.

 

Kiongozi huyo mstaafu amesema sababu za kuzindulia kitabu hicho nchini Tanzania ni kutokana na mapenzi yake ya Watanzania ikiwa pamoja na kusoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia mwaka 1968.

Hafla hizo ilihudhuliwa na wadau mbalimbali wa sheria nchini ikiwa Majaji waastaafu, majaji wa Mahakama ya Tanzania na mawakili mbalimbali.

error: Content is protected !!