Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Jaji Mkuu Rasmi Kuanza Kazi
Habari Mchanganyiko

Jaji Mkuu Rasmi Kuanza Kazi

Jaji Mkuu wa Tanzania, Ibrahim Hamis Juma akila kiapo
Spread the love

Rais wa Tanzania  Dkt John Mgufuli, amemwapisha Jaji Mkuu wa Tanzania, Ibrahim Hamis Juma, ambapo awali alikuwa akikaimu nafasi alikuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, baada ya aliyekuwa Jaji Mkuu kustaafu kisheria, Mohamed Othman Chande, anaandika Irene david.

Akizungumza leo na waandishi wa habari katika shughuli za kuapishwa zilizofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Jaji Ibrahim amesema ataendeleza misingi mizuri waliyoiacha majaji wakuu waliopita ikiwemo kupambana na rushwa katika taifa na pia kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa mahakama katika mikoa mbalimbali nchini.

Aidha ameongezea kwa kusema kuwa atasimamia haki kama sheria inavyoitaka Mahakama kutoa haki kwa raia wote nchini.

“Tatizo la uhaba wa mahakama ya mwanzo nchini imekuwa ni changamoto na kwamba tayari mikakati ilishawekwa na Jaji aliyepita hivyo kilichobaki ni utekelezaji na kuwa utafanikiwa mpango huo,” amesema Jaji Ibrahim.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!