Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari Jaji Mkuu awaonya mawakili wanaoshambulia mitandaoni
Habari

Jaji Mkuu awaonya mawakili wanaoshambulia mitandaoni

Spread the love

 

JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, amewaonya mawakili wanaotumia mitandao ya kijamii, kushambulia utendaji wa mahakama na uamuzi unaotolewa na majaji. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Prof. Juma onyo hilo leo Ijumaa, tarehe 10 Desemba 2021, akihutubia katika sherehe ya 65 ya kuwakubali na kuwapokea mawakili wapya 313, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Kiongozi huyo wa mahakama, amesema mawakili hao aliowataja kwamba wanashambulia mitandaoni kama nyuki, anawafahamu na kuwa siku zao zinahesabika.

“Tumewashuhudia leo mkiinama kwa heshima kwa jopo na kwa jaji mkuu, sasa huko kuinama huwa kunaisha mkiingia katika mitandao ya kijamii, manashambulia kama nyuki. Kwa bahati nzuri majina yenu mengine ya kibandia nayajua,” amesema Prof. Juma.

Prof. Juma “huwa najua huyu ni wakili fulani anamshambulia jaji kwa jina, wakati mwingine yuko mahakamani kesi inaendelea anamshambulkia wakili wa upande wa pili. anamshabulia jaji lakini tunawafahamu, sasa siku zao zimekwisha.”

Prof. Juma amesema, mawakili wanaowashambulia majaji na mahakimu mitandaoni kwa kuwataja majina yao pamoja na kuweka picha zao, hawastahili kuendelea kuwepo katika orodha ya mawakili.

“Lakini mawakili wamechukua hatua kesi ikienda dhidi yao, wanamshambulia jaji na hakimu kwa jina na kwa picha. Mnaweka picha yake jaji huyu wapi anaishi, hiyo haikubaliki huyo wakili hastahili kuwa katika orodha ya mawakili,” amesema Prof. Juma.

Hata hivyo, Prof. Juma amesema, wakili anaruhusiwa kukosoa maamuzi au hukumu inayaotolewa na mahakama , lakini kwa kuzingatia taatibu zilizopo.

“Ninyi mawakili ni maafisa wa mahakama, mnatakiwa kutetea uhuru wa mahakama na vilevile kuwasaidia wananchi wawe na imani kwa mahakama. Bahati mbaya baadhi yenu badala kukosoa maamuzi sababu kukosoa maamuzi ni haki yako,” amesema Prof. Juma.

Wakati huo huo, Prof. Juma amewaonya mawakili wanaowatoza fedha wateja wao kinyume cha sheria.

“Baadhi ya mawakili huwatoza wateja wao fedha zaidi, kwa madai sehemu ya hizo fedha hupelekwa kama mgawo wa majaji ama hakimu, sisi hatuchukui mgawo hata siku moja. Lakini wapo mawakili wanataka zaidi ya sheria inavyotamka, akisema hii ni ya kamati yake ya ufundi ya kupeleka kwa jaji,” amesema Prof. Juma.

Kiongozi huyo wa mahakama, ametoa wito kwa wananchi kuwaripoti mawakili wanaowatoza fedha kinyume cha sheria.

“Mwananchi ukikutana na wakili wa namna hiyo tuletee, tutamfuta dakika hiyo sababu majaji bahati nzuri wana mamlaka papo kwa papo, anakusimamisha na ningeomba sana majaji tutumie hayo mamlaka yetu kurudisha nidhamu,” amesema Prof. Juma.

Lakini kuna mawakili wenye vyeti, mavazi wapo. Kuna tatizo la maadili bado lipo. Wananchi wanalalamika lakini hatuchukui hatua yoyote.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amesema, ndani ya mwezi mmoja, baada ya kuanza kazi Kituo Jumuishi cha Temeke, asilimia 38 ya mashauri yaliyofunguliwa na mawakili, “yalirejeshwa kwao, makosa kama kutaja kifungu cha sheria. Majaji tuangalia la kufanya ili tusiwe tunawarudishia tu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariHabari Mchanganyiko

CRB yashtukia makandarasi wanaofanya ubia wa ujanja ujanja, yasema watakaobainika kuchukuliwa hatua kali

Spread the love  BODI ya Usajili wa Makandarasi (CRB), imeonya makandarasi wanaofanya...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

Habari

Mnyika aacha ujumbe msibani kwa kada wa Chadema aliyefia vitani Ukraine

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Taifa, John...

HabariHabari Mchanganyiko

Mwili wa kada wa Chadema aliyefia vitani Ukraine wawasili, kuzikwa Mbeya

Spread the loveMWILI wa Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, aliyefia...

error: Content is protected !!