February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Jaji Mkuu akamatwa kwa ufisadi

Philomena Mwilu, Naibu Jaji Mkuu wa Kenya

Spread the love

PHILOMENA Mwilu, Naibu Jaji Mkuu wa Kenya amekamatwa na vyombo vya dola kwa tuhuma za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Taarifa hizo zimethibitishwa na Noordin Haji, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Kenya wakati akizungumza na wanahabari leo tarehe 28 Agosti, 2018 ambapo amedai kuwa, kuna ushahidi wa kutosha unaomtia hatiani Jaji Mwilu.

Haji amesema Jaji Mwilu amefunguliwa mashtaka ya uhalifu katika mahakama kuu iliyoko mjini Nairobi nchini Kenya.

Tukio hilo ni muendelezo wa serikali ya Kenya katika kutekeleza mkakati wake wa kupambana na vitendo vya ufisadi na rushwa kwa viongozi na watumishi wa umma nchini humo.

error: Content is protected !!