Friday , 1 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Jaji Kiongozi akerwa wananchi kukosa imani na mahakama
Habari za Siasa

Jaji Kiongozi akerwa wananchi kukosa imani na mahakama

Jaji Kiongozi, Mustapha Siyani
Spread the love

WATENDAJI wa Mahakama ya Tanzania, wametakiwa kuweka mikakati itakayosaidia kurejesha imani ya wananchi kwa mahakama, ili kuimarisha utoaji haki nchini. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 11 Disemba 2023, jijini Dar es Salaam na Jaji Kiongozi, Mustapha Siyani, katika hafla ya kuwaapisha manaibu wasajili wa mahakama hiyo.

“Nikisia sauti za watu ni hiki kinachosemwa hatuna imani na mahakama, imani ndiyo mtaji wa mahakama jamii yetu isipokuwa na imani na vyombo hivi vya kutolea haki hususan mahakama haitavitumia na isipovitumia upo uwezekano wa nchi yetu kuingia kwenye machafuko, Mnao wajibu mkubwa kuhakikisha mnasimamia na kutekelza mpango mkakati kuimarisha imani ya umma kwa mahakama,” alisema Jaji Siyani.

Katika hatua nyingine, Jaji Siyani amewataka watendaji wa mahakama hususan viongozi, kutotumia madaraka yao vibaya.

“Msilewe madaraka, madaraka ni kitu chepesi kinacholevya kwa haraka kuliko kilevi chochote. Msipojizuia kidogo ni rahisi sana mkajikuta mmelewa,” amesema Jaji Siyani.

Kwa upande wake, Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, amewataka watendaji hao watekeleze majumu yao pasipo kusubiri maelekezo kutoka viongozi wa juu.

“Mkiangalia sheria ya uendeshaji wa mahakama imeweka matumaini makubwa na manaibu wasajili, kwamba hii kada ya viongozi ni muhimu sana, imetumika kutoa uhuru mkubwa kutimiza majukumu yenu bila kusubiri maelekezo au kupewa maagizo katika majukumu ambayo tayari mmepewa kisheria. Inabidi mfanye kazi bila kusubiri maelekezo,” alisema Prof. Juma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

Habari za Siasa

Waziri mkuu Ethiopia atua Tanzania

Spread the loveWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia,...

Habari za Siasa

Babu Owino: Vijana msibaki nyuma

Spread the loveMbunge wa Embakasi Mashariki nchini Kenya, Paul Ongili Owino maarafu...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia: Hatutazuia watu kuingia barabarani

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali itaendelea kuruhusu vyama...

error: Content is protected !!