January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jaji Chande: Mahakama ngono tupu

Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu, Chande Othman

Spread the love

CHAMA cha Majaji wanawake Tanzania (TAWJA), kimeazisha mtandao maalumu wa kupambana na rushwa ya ngono zinazoshamiri katika sekta ya umma, anaripoti Sarafina Lidwino.

Miongoni mwa maeneo ambayo rushwa ya ngono imedaiwa kuota mizizi, ni Mahakama, Bunge na Polisi.

Jaji Mkuu Chande Othman amewaambia waandishi wa habari kuwa muhimili wa mahakama utashirikiana na taasisi hiyo kukomesha vitendo hivyo.

“Mahakama inatambua mchango mkubwa unaotokana na taasisi hii, ikiwamo mapambano ya kupigania haki za watoto, wanawake na usawa katika maendeleo ya jamii,” amesema Jaji Chande.

Jaji Chande alikuwa akifungua semina ya majaji wanawake juu ya rushwa ya ngono katika maeneo yanayotoa huduma kwa umma.

Amesema, “Mafunzo haya ni muhimu katika jamii. Yanakuza na kuendeleza haki za binadamu katika taifa na utawala wa sheria. Mafunzo haya yatasaidia sana kuwajengea uwezo majaji kutekeleza majukumu yao.”

Amewataka watu wengine kupambana na rushwa ya ngono, aliyokiri imechangia kupindisha haki kutendeka, kuungana na taasisi hiyo, katika kusaidia mahakama kupambana na rushwa ya ngono.

TAWJA ambayo inaongozwa na Jaji Angera Kileo, imechapisha vipeperushi mbalimbali vinavyokataza matumizi mabaya ya madaraka.

Jaji Chande amesema, TAWJA imedhihilisha kuwa wanawake wanaweza kuleta mabadiliko katika jamii.

“Natoa wito kwa wananchi wote kuweza kushirikiana  Mahakama Kuu na TAWJA katika kuyapatia ufumbuzi matatizo ya rushwa ya aina yoyote ile haswa katika mahakama. Katika mahakama, hatutojali kuwa una cheo gani; sheria itachukuwa mkondo wake,” amesisitiza.

Jaji Chande alisema tatizo la ngono nchini ni kubwa. Akatoa mfano wa askari mmoja wa jeshi la polisi mkoani kuwa aliomba ng’ono kwa mtoto wa miaka 12 ambaye alifikishwa kituoni akituhumiwa kwa baadhi ya makosa.

Alisema, binti huyo kwa kuhofia polisi, alilazimika kukubaliana na kitendo hicho, jambo ambalo lilisababisha mtoto huyo kupata matatizo makubwa katika “uuke wake.” Askari huyo amehukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani.

Mkutano ambako Jaji Chande alitoa kauli hiyo, umefanyika katika hoteli ya New Africa jijini Dar e s Salaam.

error: Content is protected !!