July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jaji atoa uamuzi kupinga uchguzi TFF

Spread the love

 

MAHAKAMA Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, imetoa mwongozo wa kesi ya zuio la uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), isikilizwe ndani ya siku saba, kuanzia leo IJumaa tarehe 3 hadi 9 Julai 2021, iwe imemalizika, kabla ya kesi ya msingi haijaanza kusikilizwa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea).

Uamuzi huo, umetolea na Jaji Kakolaki baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote katika kesi hiyo iliyofunguliwa na Ally Saleh ‘Alberto’ ambaye alikuwa moja ya wagombea urais wa TFF.

Jaji Kakolaki amesema, maombi hayo madogo yanapaswa kusikilizwa ndani ya kipindi hicho.

Uchaguzi huo umepangwa kufanyika tarehe 8 Agosti, 2021, jijini Tanga, ambapo mpaka sasa kamati ya uchaguzi imempitisha Wallace Karia kuwa mgombea pekee kwenye nafasi ya Urais. Karia ni rais wa shirikisho hilo kwa sasa.

Kesi hiyo ya madai namba 98 ya mwaka 2021, iliyofunguliwa na Ally Salehe, raia wa Tanzania anayeishi Zanzibar ambayo itakuwa chini ya Jaji Kakolaki ambapo wadai ni TFF, Bodi ya wadhamini na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Wakili Kiomoni Kibamba.

Frank Chacha, wakili wa Saleh amesema, mteja wake amefungua kesi mbili katika Mahakama Kuu hiyo akiomba mahakama hiyo, isimamishe shughuli zote za uchaguzi kwa sabahu umekuwa ukikiuka haki ya vyama vya mpira vya Zanzibar.

Alisema, Saleh amefungua kesi hiyo kwa kuwa uchaguzi huo, haukufuata kanuni hasa kwenye ibara ya 30 inayoonekana kubagua wagombea kutoka Zanzibar.

Katika kesi hiyo, Saleh ana mawakili wawili, Frank na Steven Mosha huku TFF ikiwa na wakili John Mushumbuzi.

error: Content is protected !!