September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Jaji anayesikiliza kesi ya kina Mbowe ajitoa, kisa…

Spread the love

 

JAJI Elinaza Luvanda, aliyekuwa anasikiliza kesi ya ugaidi inayomkabili Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Freeman Mbowe na wenzake amejitoa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Amechukua uamuzi huo leo Jumatatu, tarehe 6 Septemba 2021, katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi baada ya Mbowe akiwakilisha wenzake kumwomba Jaji Luvanda ajitoe.

Ni baada ya mapingamizi yao matatu kati ya manne waliyokuwa wameweka dhidi ya hati ya mashtaka iliyutumika kuwafungulia mashtaka kutupiliwa mbali.

Mbowe amesema, kesi hii imeleta hisia kwa jamii na inawexa kuthibistishwa na mijadala inayoendelea mitandaoni.

Amesema, mijadala hiyo haiwezi kupuuzwa ikiwemo taarifa zinazosema nanukuu “Jaji Luvanda ni Mserikali na TISS yupo mahakama ya mafisadi kimkakati ameelekezwa kumfunga Mbowe huku msajili akishughulika na Chadema”

Rais atamuachia baada ya muda. Kila pingamizi atalitupilia mbali haijalishi uhalali wake,” amesema Mbowe na kuongeza:

“Naomba niishie hapo katika kunukuu. Jaji haya maneno au hisia za jamii hatuwezi kupuuza ni ombi langu Jaji ikikupendeze kujitoa katika shauri hili ili kujenga heshima yako na ya mahakama ili usibebeshewe lawama ambayo si sahihi.”

Mara baada ya Mbowe kumaliza kuwasilisha maombi yake, Jaji Luvanda akasema “nimesikia hoja za pande zote mbili niseme msingi wake ni suala la dhana kuliko uhalisia ulivyo. Sina sababu ya kujitetea na siwezi kujitetea katika jambo ambalo kimsingi halipo.”

“Iwa kuzingatia kwamba shauri lina maslahi kwa umma nilete jaji mwingine kuendelea na shauri. Nichukue nafasi hii kuwashukuru wote,” amesema Jaji Luvanda na kuahirisha kesi hiyo hadi atakapopangiwa kazi mwingine

error: Content is protected !!