Sunday , 2 April 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Jafo atangaza waliochaguliwa kidato cha kwanza 2021
Habari MchanganyikoTangulizi

Jafo atangaza waliochaguliwa kidato cha kwanza 2021

Suleiman Jafo, Waziri wa Tamisemi
Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imesema, wanafunzi 759,706 sawa na asilimia 91.1 ya wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba 2020, wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwaka 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Kati yao, wavulana 368,174 na wasichana 391,532.

Hayo yamebainishwa leo Alhamisi tarehe 17 Desemba 2020 mbele ya waandishi wa habari na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemama Jafo.

Amesema, kati yao, wanafunzi 4,169 wamechaguliwa kujiunga na shule za bweni ambapo wanafunzi 970 watajiunga na shule za wanafunzi wenye ufaulu mzuri zaidi. Wanafunzi 1,238 watajiunga na shule za ufundi, wanafunzi 1,961 watajiunga na shule za bweni za kawaida.

Waziri Jafo amesema, wanafunzi 755,537 wakiwemo wavulana 362,247 na wasichana 385,665 wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari za kutwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Amesema, miongoni mwa waliochaguliwa, wanafunzi wenye mahitaji maalum ni 2,491 wakiwemo wavulana 1,312 na wasichana 1,179 sawa na asilimia 75.0 ya wanafunzi wenye ulemavu waliofanya mtihani huo.

Waziri Jafo ameitaja mikoa tisa iliyoweza kuwapangia wanafunzi wote waliochaguliwa awamu ya kwanza.

Ameitaja mikoa hiyo ni; Kagera, Katavi, Lindi, Mtwara, Njombe, Mwanza, Songwe, Ruvuma na Tabora “nawapongeza sana viongozi wa mikoa hii kwa kuwapangia kwenye awamu ya kwanza.”

Soma zaidi: 

Matokeo darasa la saba 2020 haya hapa

Jafo amesema, wanafunzi 74,169 sawa na asilimia 8.9,  wavaluna  34,861 na wasichana 39,305 hawakupangiwa shule katika awamu ya kwanza kutokana na ubaha wa madarasa.

“Watapangiwa awamu ya pili kabla ya tarehe 28 Februari 2020 na malengo ya Serikali, wanafunzi wote waliofaulu watajiunga katika awamu ya pili,” amesema

Jafo amesema, kwa mara ya kwanza, uchaguzi wa wanafunzi umefanyika kwa njia ya kielektroniki na kama mzazi au mlezi ana tatizo “afike kwenye ofisi zetu za mikoa au apige namba 0262160210 au atume ujumbe mfupi kwenye namba 0735160210.”

“Hatutabaki na mtoto ambaye hatajiunga na Sekondari na watoto wote watajiunga na sekondari. Hii ni neema, wanafunzi kufaulu wengi hivi, sisi ni mafanikio makubwa,” amesema Jafo

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Ditopile aungana na Wana-Kongwa kwa Iftar, wamuombea dua Rais Samia

Spread the loveKATIKA muendelezo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Mbunge wa Viti...

Habari Mchanganyiko

PSSSF yawekeza kwenye viwanda 4, kuzalisha ajira 3,000

Spread the loveKATIKA kuisaidia Serikali kupunguza tatizo la uhaba wa ajira nchini,...

Habari Mchanganyiko

Luhemeja ahimiza utunzaji rasilimali maji kwa faida ya vizazi vijavyo

Spread the love  NAIBU Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja...

Habari Mchanganyiko

NSSF yawapa darasa wahariri uwekezaji wa nyumba, yapewa cheti

Spread the loveMFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umetoa wito...

error: Content is protected !!