Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Jafo ataka utafiti wa bioteknolojia
Habari Mchanganyiko

Jafo ataka utafiti wa bioteknolojia

Spread the love

OWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Suleiman Jafo amewataka watafiti na wataalamu waliojikita kwenye teknolojia ya bioteknolojia kufanya tafiti ambazo zitawezesha jamii kupata uelewa na kuondoa hofu iliyopo kuhusu teknolojia hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Waziri Jafo amesema hayo leo tarehe 25 Oktoba, 2022 kwenye ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Chama cha Bioteknolojia Tanzania (BST) uliofanyika katika ukumbi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) jijini Dar es Salaam.

Dk Jafo amesema kumekuwa na mkakanganyiko kuhusu bidhaa zinazotokana na bioteknolojia hapa nchini, hivyo njia ya kuondoa hali hiyo ni vema watafiti wakafanya tafiti za kina ambazo zitaiwezesha Serikali kuchukua hatua stahiki.

Amesema taarifa zinaonesha bioteknolojia inatumika kwenye sekta ya afya, viwandani, kilimo na kwingineko ila upingaji au uungaji mkono umejikita katika kilimo hali ambayo inaibua malumbano kila kukicha.

“Sisi Serikali hatuna shida na tafiti kuhusu bioteknolojia, ila msukumo mkubwa utaonekana iwapo tafiti zitafanyika ili kuhakikisha kundi ambalo linapinga ua halina uelewa liweze kuelewa, kwani haiwezekani hata nguo ambazo tunavaa zinatoka na bioteknolojia, lakini wapo watu wanapinga, lazima elimu ya kutosha itolewe,” amesema.

Waziri Jafo amesema wapo watu ambao wanahusisha  bioteknolojia na masuala ya mabadiliko ya tabianchi yaliyopo kwa sasa, hivyo yote hayo ili kuondoa hiyo dhana tafiti na elimu ni muhimu.

Awali akizungumza kwenye mkutano huo wa kwanza wa Mwenyekiti wa BST, Profesa Peter Msolla amesema, matumizi ya bioteknolojia duniani yameleta manufaa makubwa kwenye sekta mbalimbali kama kilimo, afya, mifugo, viwanda na mazingira.

“Bioteknolojia imewezesha uzalishaji wa miche isiyo na vimelea vya magonjwa, mazao bora yasiyoshambuliwa na  visumbufu vya magonjwa na wadudu, pamoja na kupunguza gharama za uzalishaji.

Katika sekta ya afya imerahisisha utambuzi wa magonjwa kwa usahihi, pamoja na utengenezaji wa chanjo na dawa mpya na zenye ubora zaidi kukabili magonjwa sugu kwa mfano insulin kwa wagonjwa wa kisukari, homa ya ini (hepatitis B), saratani ya shingo ya kizazi, magonjwa ya kuhara kwa watoto, na chanjo za VVU/Ukimwi na Uviko-19,” amesema.

Amesema utafiti unaendelea wa kutumia teknolojia hiyo katika kuzuia au kutokomeza ugonjwa wa malaria.

Prof Msola amesema hali kama hiyo imeonekana kwenye  sekta ya mifugo kwa kurahisisha utambuzi wa magonjwa kwa usahihi, kuongeza uzalishaji wa aina bora za mifugo, pamoja na utengenezaji wa dawa na chanjo;

“Katika sekta ya viwanda bioteknolojia imeweza kuongeza ufanisi na tija katika kutengeneza bidhaa mbalimbali za vyakula, pamoja na madawa na kemikali kwa matumizi ya kilimo na viwandani bila kuharibu mazingira,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!