July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jafo afanya ziara ya kushtukiza sokoni

Spread the love

NAIBU Wazari wa TAMISEMI, Seleman Jafo jana alivamia soko Kuu la Majengo mjini hapa na kuanza kukagua stakabadhi za ushuru kwa wafanyabiashara wa soko hilo kama zimetolewa kwa mfumo wa kieletroniki, anaandika Dany Tibason, Dodoma.

Jafo alifika sokoni hapo huku akifuatana na Meckiloh Komba, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma na Rehema Madenge, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma.

Mara baada ya Jafo kufika alionana na uongozi wa soko hilo na hivyo baada ya kuongea nao aliwaoomba waende kutembelea wafanyabiashara hao.

Alipofika alianza kuomba stakabadhi hizo na kuona kama ni kweli zimetolewa kwa mfumo huo.

“Nasema kama unatoa fedha zako za ushuru usikubali kupewa stakabadhi ambayo si ya kieletroniki huko ni kuibia serikali,’’ amesema.

Jafo alielekeza uongozi wa soko hilo kuhakikisha kuwa wafanya biashara wote wanaofanya biashara katika soko hilo wanalipa ushuru kama ilivyopangwa.

“Kuna wengine nimewakuta nje wakiuza bidhaa zao chini je wale wanalipa ushuru huko ni kuwaonea wengine waliopo humu ndani hivyo wale nao wafanyiwe utaratibu utakao wawezesha kulipa kodi siyo mwingine analipa mwingine halipi huku wanafanya biashara ya aina moja,’’ amesema.

Awali akizungumza na Waziri Jafo, mwenyekiti wa Soko hilo Godson Rugazama amesema soko hilo linakabiliwa na tatizo na paa kuvuja .

Amesema hata hivyo waliwasiliana na Manispaa ya Dodoma katika kuhakikisha suala hilo linapatiwa ufumbuzi wa haraka.

error: Content is protected !!