May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jafo aagiza wanafunzi kupanda miti milioni 14

Spread the love

 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Seleman Jafo amewaagiza maofisa mazingira nchini kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu kuhakikisha wanapanda miti milioni 14 ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Pia amewaagiza maofisa mazingira nchini kuisimamia kampeni hiyo kwa kwenda katika shule na vyuo mbalimbali kuikagua miti hiyo ambayo itakuwa imepandwa. Anaripoti Danson Kaijage – Dodoma… (Endelea)

Waziri Jafo ametoa kauli hiyo jana tarehe 20 Januari, 2022 wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na Vyuo nchini yenye kauli mbiu ‘Soma na Miti’ amesema lengo ni kila mwanafunzi wa shule ya msingi, sekondari na chuo apande mti.

“Pia wizara ya elimu iliangalieni hili kwamba kupitia kila mwanafunzi anayechukua mkopo kule Bodi ya Mikopo wapande miti maana ukame unazidi kuongezeka,” ameongeza.

Jafo amesema wanafunzi waliopo katika shule za msingi na sekondari jumla wapo milioni 14.1 hivyo wamepanga kila mwanafunzi apande mti mmoja ili kufikisha idadi hiyo na kwa upande wa vyuo vya kati na vyuo vikuu kuna jumla ya wanafunzi 400,000 ambao nao wote watapanda miti.

Ameeleza kuwa ukosefu wa mvua katika siku za hivi karibuni unasababishwa na mabadiliko ya tabia nchi na kwamba kuna haja ya kuhakikisha mazingira yanatunzwa ikiwa ni pamoja na miti kupandwa.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia elimu, David Silinde ameagiza kufufuliwa kwa klabu za utunzaji wa mazingira katika shule.

Pia ameagiza maofisa elimu kuzisimamia kwa vitendo kampeni ya soma na mti kuhakikisha inatekelezwa kikamilifu.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka aliwataka wale wenye viwanja vipya kupanda miti mitatu katika viwanja hivyo ikiwemo wa kivuli na mti mmoja na miwili ya matunda.

“Agenda ya utunzaji wa mazingira katika Mkoa wa Dodoma ni kampeni endelevu,” amesema Mataka.

Wakati Meneja wa miradi wa Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori (WWF), Tanzania Dk. Severin Kalonga amesema ofisi yao imekuwa ikifanya kazi zaidi ya miaka 25 hapa nchini katika maeneo ya misitu, wanyamapori, vyanzo vya maji kwamba wadau wao wakubwa ni serikali.

error: Content is protected !!