Sunday , 25 February 2024
Home Habari Mchanganyiko Jaffo azitaka halmashauri kupima maeneo
Habari Mchanganyiko

Jaffo azitaka halmashauri kupima maeneo

Suleiman Jaffo, Naibu Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Spread the love

SERIKALI imeziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinapima ardhi kwa lengo la kuondokana na migogoro ambayo ambayo imekuwa ikijitokeza katika maeneo mbalimbali, anaandika Dany Tibason.

Licha ya serikali kuziagiza halmashauri kuagizwa kupima ardhi,pia halmashauri zimeelekezwa kutumia ofisi za wenyekiti wa vijiji na mitaa ambazo kwa sasa zimekuwa zikitumiwa na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kauli hiyo ilitolewa leo Bungeni na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEM, Selemani Jafo alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalum Cecilia Paresso (Chadema)alipokuwa akitaka kujua nini adhima ya serikali katika kuondoa migogoro ambayo inajitokeza kwa serikali kuvamia viwanja vya shule.

Awali katika swali la msingi la mbunge wa Viti Maalum,Upendo Peneza (Chadema)ambaye alitaka kujua ni lini serikali itafanya uchunguzi na kurudisha maeneo ambayo ni mali ya Umma lakini yamekuwa yakiporwa na Chama cha Mapindizi CCM.

Akijibu swali la nyongeza Jafo alisema yapo maeneo ambayo ya awali zilikuwa zikitumiwa na wanyeviti wa serikali za Mitaa na Vijiji,wakiwa CCM na ofisi hizo zilikuwa zilikuwa na nembo ya CCM, lakini kutokana na kutokuwa na nafasi kwa sasa wanatakiwa kuachia maeneo hayo na ifahamike kuwa kwa sasa ofisi hizo ni za serikali za mitaa.

“Najua zilikuwepo ofisi ambazo zilijengwa na CCM na kuwekewa nembo ya CCM,lakini ofisi hizo zilijengwa katika maeneo ya viwanja vya Serikali za Mitaa na Vijiji kwa maana hiyo zinatakiwa kutumiwa na wenyeviti waliopo madarakani kwa sasa na nimeisha toa maelekezo kwa halmashauri zote nchini zenye matatizo kama hayo”alisema.Jafo.

“Kumekuwepo na uporwaji wa maeneo ya Umma kama vile maeneo ya Shule Kalangalala na maeneo ya Serikali za Mitaa.

“Je ni lini serikali itafanya uchunguzi na kurudisha maeneo hayo kwa Umma”alihoji Paresso.

Akijibu maswali hayo Jafo alisema ni kweli wapo wananchi wanne ambao wamevamia eneo la shule ya Sekondari Kalangala iliyoko halmashauri ya Mji wa Geita ambao walijenga nyumba zao ndani ya mchoro wa mpango mji wa eneo la shule.

Halmashauri kwa kushirikiana na mkoa imepanga kuwaondoa wananchi hao waliovamia na kujenga kwenye eneo la shule na maelekezo yametolewa kwa halmashauri zote nchini kuhakikisha maeneo yote ya Umma yanapimwa na kupatiwa hati miliki yakiwemo shule,vituo vya kutolea huduma za afya na maeneo ya wazi yaliyotengwa kwa matumizi mbalimbali ya Umma.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

25 wafariki dunia katika ajali Arusha

Spread the loveWatu 25 wamefariki dunia papo hapo mkoani Arusha katika ajali...

Habari Mchanganyiko

“Jamii ielimishwe faida za uhifadhi”

Spread the loveWIZARA ya Maliasili na Utalii imesema ili kukabiliana na migongano...

Habari Mchanganyiko

Shahidi aeleza Nathwani alivyomshambulia jirani yake

Spread the loveSHAHIDI ambaye ni fundi Seremala, Dominic Mpakani (43) ameileza mahakama...

Habari Mchanganyiko

DCEA, TAKUKURU waunganisha nguvu kupamba na dawa za kulevya, rushwa

Spread the love  MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya...

error: Content is protected !!