August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jaffo ‘ayananga’ maonesho ya nanenane

Suleiman Jaffo, Naibu Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

Spread the love

NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), Selemani Jafo amewashukia, Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa mikoa ya Dodoma na Singida kwa kushindwa kufanya maandalizi ya uhakika ya Nane nane kanda ya kati, anaandika Dany Tibason.

Jafo amesema kuwa inasikitisha kuona maonesho ya nanenane yanageuzwa kuwa soko la kuuza nguo za ndani na mabeseni ya kuogea watoto badala ya kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji.

Jaffo amesema hayo wakati wa kilele cha maadhimisho ya wakulima nanenane kanda ya kati yaliyofanyika katika kiwanja cha Nzuguni mjini hapa.

Akifunga madhimisho hayo amesema lengo la kuwepo kwa nane nane ni kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji ili kuwawezesha kutoa elimu bora kwa wakulima kulima kilimo chenye tija badala ya kile cha kijikimu.

Amesema haiwezekani maonesho ya nane nane ambayo yapo kwa ajili ya kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji yakageuzwa kuwa sehemu ya kuuza beseni za kuogeshea watoto pamoja na kuuza nguo za ndani na mitumba.

error: Content is protected !!