June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jaffo ataka Magufuli aungwe mkono

Spread the love

MBUNGE wa jimbo la kisarawe Selemani Jaffo (CCM) amesema kasi ya rais John Magufuli inatakiwa kuungwa mkono na yoyote atakaye kwamisha spidi hiyo achukuliwe hatua. Anaandika Dany Tibason, Dodoma …. (endelea).

Jaffo watumishi ambao wamekuwa wakijilimbikizia mali ni bora mali zao zikakaguliwa na iwapo itabainika haziendani na kipato chako ataifishwe mali hizo.

Aliongeza kuwa kwa sasa hakuna sababu yoyote ya kuendelea kuwabembe watumishi ambao walitumia nafasi zao kujinufaisha.

“Kimsingi nampongeza  Magufuli kwa kasi yake hiyo natamani kasi hiendelee ndani ya miaka mitano ili kulijengea heshima taifa.

“Siyo kweli kwamba Tanzania ni masikini lakini watanzania wanaendelea kuwa masikini kutokana na baadhi ya viongozi wachache kujilimbikizia mali”alisema Jaffo.

Mbali na hilo aliwataka wanasiasa hususani vijana kuhakikisha wanaisimamia serikali badala ya kuwa na mapenzi yaliyopitiliza katika chama.

“Tumefika hapa tulipo kwa sababu ya kuwa na mahaba na ushabiki wa chama badala ya kuisimamia serikali na wakati mwingine tumekuwa na tabia ya kulindana jambo ambalo ni hatari kwa taifa.

“Sasa umefika wakati wa kukimbia kwa spidi ya rais bila kuoneana haya ili kuhakikisha heshima ya nchi inarudi maali pake,wapo watushi wengi ambao wamejigeuza kuwa miungu watu na wanatumia fedha nyingi kujinufaisha huku baadhi ya watanzania kukikabiliwa na dhiki kubwa”amesema.

error: Content is protected !!