Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Jaffar Haniu ashiriki Baraza la Madiwani Busokelo, akagua miradi ya maendeleo
Habari za Siasa

Jaffar Haniu ashiriki Baraza la Madiwani Busokelo, akagua miradi ya maendeleo

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu
Spread the love

MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu ameshiriki Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe sambamba na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Akitoa salamu za Serikali katika baraza hilo, Haniu ameishukuru Halmashauri hiyo kwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa ufanisi na kuagiza wakandarasi ambao hawajamaliza hiyo kufanya hivyo kwa wakati ili wananchi wapate huduma stahiki na Kwa wakati.

Wakati huohuo, Haniu ameaagiza watalamu mbalimbali katika halmashauri hiyo kukusanya mapato ya Serikali kwa bidii huku akiomba madiwani kuendelea kumulika vyanzo vya mapato katika maeneo yao ili kusaidia kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Aidha ameliomba baraza hilo kusimamia kwa ukaribu utoaji wa mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ikiwa ni asilimia kumi ya mapato ya ndani ya halmashauri hiyo.

Haniu ameongeza kuwa mikopo hiyo hutolewa na Serikali ili kuinua kiwango cha pato kwa wananchi hivyo Halmashauri haina budi kutoa kwa wakati na kusimamia urejeshwaji wake ili iwanufaishe na wengine.

Katika hatua nyingine, Haniu ameeleza kuwa Serikali imekuwa ikihamasisha wazazi kuhakikisha wanawapeleka watoto wenye umri wa kujiunga na elimu ya msingi sambamba na kidato cha kwanza hivyo kila mzazi na jamii kwa ujumla ina wajibu wa watoto wote wanaenda shule.

Halmashauri ya Busokelo mpaka sasa wanafunzi wa kidato cha kwanza wameripoti kwa asilimia 92% na darasa la kwanza asilimia 103%.

Aidha ameshukuru shule zote zinazotekeleza zoezi la chakula cha mchana kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na kuagiza wazazi wote ambao hawajaanza kutekeleza zoezi hilo kuanza kufanya hivyo ili kuondoa udumavu na utapiamlo kwa wanafunzi na kuongeza ufaulu shuleni.

Akizungumzia migogoro ya Ardhi, Haniu amekea migogoro inayoendelea katika ngazi ya kaya na jamii na kuwa utatuzi uendelee kwa kufuata taratibu zilizowekwa kwa kuwashirikisha viongozi, na Baraza la Ardhi.

“Migogoro mingi inatoka ngazi ya kaya ni vema suluhisho lake pia likaanzia ngazi ya kaya badala ya kugombana na kuhatarisha amani katika jamii,” amesisitiza Haniu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!