May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jacob Zuma wa Afrika Kusini ajisalimisha gerezani

Jacob Zuma

Spread the love

 

JACOB Zuma (79), Aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, ameanza kutumikia kifungo cha miezi 15 gerezani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ni baada ya Mahakama nchini humo, Jumanne ya tarehe 29 Juni 2021, kumhukumu kifungo hicho, baada ya kumtia hatiani kwa kukaidi agizo la kufika mahakamani kuhudhulia kesi inayomkabili ya ufisadi wakati alipokuwa rais.

Baada ya umuauzi huo, wafuasi wake walizunguka makazi yake wakizuia asikamatwe, jambo lililowafanya ujumbe wa polisi kufika nyumbani kwake, Jimbo la Kwazulu Natala.

Katika mazungumzo yao, walikubaliana kwamba Zuma ajisalimishe yeye mwenyewe na alitii wito huo na jana Jumatano, tarehe 7 Julai 2021, akisindikizwa na walinzi wake, alikwenda katika gereza lililokaribu na nyumbani kwake.

Polisi nchini humo wamethibitisha Zuma kujisalimisha huku baadhi ya wafuasi wake, waliokuwa wamekusanyika nyumbani kwake, wakionesha kutofurahishwa kwa kiongozi huyo wa zamani wa Afrika Kusini, kuhukumiwa kifungo gerezani.

error: Content is protected !!