RAIS wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ameachiliwa kwa dhamana katika gereza la Estcourt mashariki mwa nchi hiyo kutokana na sababu za kiafya hazikuelezwa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Mamlaka ya magereza nchini humo ilitangaza tarehe 5 Septemba, 2021 kuwa kiongozi huyo amelazwa hospitalini kwa muda wa mwezi mmoja sasa.
Zuma (79), amekuwa akitumikia kifungo cha miezi 15 jela kwa kudharau mahakama tangu Julai mwaka huu, baada ya kukataa kufika mbele ya tume inayochunguza ufisadi chini ya utawala wake.
Kwa mujibu wa mamlaka ya magereza, uamuzi huo umechukuliwa baada ya kupokea ripoti ya matibabu yake.
Zuma pia anashtakiwa katika kesi ya ‘Thales’, kesi nyingine ya ufisadi iliyoanzia mwishoni mwa miaka ya 1990.
Wakati kesi yake imepangwa kuanza tena Alhamisi wiki hii, Zuma amekataa kuendelea kuchunguzwa ilihali sasa amelazwa hospitalini.
Kufungwa kwake kulisababisha ghasia kadhaa na visa vya uporaji nchini humo hali ambayo ilisababisha vifo vya zaidi ya watu 350 mwezi Julai mwaka huu.
Leave a comment