Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko DC Dodoma: Tusisubiri kusukumwa kufanya usafi
Habari Mchanganyiko

DC Dodoma: Tusisubiri kusukumwa kufanya usafi

Spread the love

MKUU wa wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri amewataka wakazi wa jiji la Dodoma kujenga tabia ya kufanya usafi kila siku badala ya kusubiri kusukumwa na viongozi wa serikali kufanya usafi wa kila ifikapo Jumamosi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma (endelea).

Shekimweri ametoa wito huo leo tarehe 23 Julai, 2022 alipokuwa akizungumzia na wafanyabiashara na wateja mbalimbaki wa Soko kuu la Majengo muda mfupi baada ya kumaliza zoezi la kufanya usafi.

Amesema yeye siyo muumini wa kukubali kufunga biashara siku ya Jumamosi ya usafi na kueleza kwa kufunga maduka kwa ajili ya kufanya usafi ni kudumaza huduma za kibiashara na kuwafanya watu kukosa huduma muhimu.

“Nataka jambo hili mlijue na ninaaka kuliwekea mkazo mimi siyo muumini wa kufunga maduka wakati wa siku ya usafi, kwa kuwa zinapofungwa sehemu za huduma athari zake ni kubwa.

“Mfano kuna mtu anaumwa anahitaji kupatiwa huduma ya kununuliwa dawa au mtu anasafiri lakini anahitaji kununua kipuri cha gari lake lakini gereji imefungwa madhara yake anapoteza muda kusubiri kufunguliwa kwa maduka muda wa saa tatu.

“Lakini tamko hilo linatekelezeka kutokana na watu kutokuwa na mwamko wa kufanya usafi katika maeneo yao, kama usafi ingekuwa desturi ya kila siku tamko hilo tungelitoa na sasa nawaasa kuhakikisha mnafanya usafi ili kuondoa tamko hilo la kufunga maduka na sehemu zote za huduma katika siku ya kufanya usafi.

” Na leo tumewakamata watu 20 na kuwatoza faini ya sh 500,000 kila mmoja kutokana na kukiuka sheria ndogo za jiji kwa kukwepa kufanya usafi na tutaendelea kuwachukulia hatua wale wote watakao kiuka sheria ndogo za jiji”ameeleza Shekimweri.

Katika hatua nyingine Shekimweri ametoa wito kwa wawekezaji kufanya mazungumzo ya mamlaka husika yaani Jiji au wilaya ili wapewe maeneo ya wazi na waone jinsi ya kuyaboresha na kuweka matangazo yao kwa nia ya kujitangaza.

Kwa upande wake Meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwanfupe amesema jiji la Dodoma linaendelea kupambana kuhakikisha linahimiza usafi wa mtu mmoja mmoja,kaya nataasisi.

Prof. Mwanfupe amesema a kwa sasa kauli mbiu ya usafi katika jiji la Dodoma ni ” hatua tano usafi wangu,usafi wangu hatua tank”.

Naye Afisa Usafi wa Mazingira Jiji la Dodoma, Dickson Kimaro amesema Jiji litaendelea kuwachukulia hatua watu ambao wamekuwa wakikiuka misingi ya usafi wa mazingira kama sheria zinavyoelekeza.

“Kutokana na hali ya Jiji ilivyo kimsingi kila mmoja unatakiwa kuhakikisha anatunza mazingira bila kusukubwa na viongozi.

” Nawaagiza mgambo wa jiji kuhakikisha mnawasaka na kuwakamata watu ambao ni wakorofi wanaozalisha uchafu na kushindwa kutekeleza sheria za utunzaji wa usafi katika maeneo yao”amesema Kimaro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

error: Content is protected !!