January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ivory Coast yatwaa taji la AFCON 2015

Wachezaji wa Ivory Coast wakishangilia ubingwa, huku wakiwa wamembeba kipa wao, Boubacar Barry

Spread the love

TIMU ya Taifa ya Ivory Coast ndiyo mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2015 baada ya kuifunga Ghana kwa penalti 9-8 kufuatia sare ya 0-0 katika dakika 120 katika mchezo wa uliochezwa kwenye Uwanja wa Bata, Guinea ua Ikweta. Anaripoti Erasto Stanslaus ….. (endelea).

Kwa ushindi huo wa Ivory Coast. historia imejirudia, baada ya timu hiyo kuifunga kwa mtindo huo tena Ghana kama ilivyokuwa katika fainali ya mwaka 1992 ambapo walishindwa kwa penalti 10-9 na kutwaa taji lao la kwanza.

Shukrani kwa kipa wa Ivory Coast, Boubacar Barry aliyepangua penalti ya mwisho ya Ghana iliyopigwa na kipa mwenzake, Razak Braimah kabla ya kukwamisha mkwaju wa mwisho na kumaliza kiu ya miaka 23 ya kusubiri taji hilo.

Penalti za Ivory Coast zilifungwa na Aurier, Doumbia, Yaya Toure, Soomon Kalou, Kolo Toure, Kanon, Bailly Serey Die na Barry, wakati Wlifried Bony na Tallo walikosa mbili za kwanza.

Penalti za Ghana zilifungwa na Mubarak Wakaso, Joedan Ayew, Andre Ayew, Mensah, Agyemang-Badu, Afful, Baba na Boye wakati Acquah, Achwampong na Brimah walikosa.

Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang, Rais wa FIFA, Sepp Blatter na Rais wa CAF, Issa Hayatou walikuwepo uwanani na awali walikagua vikosimkabla ya kukabidhi Medali na taji kwa washindi baada ya mechi.

error: Content is protected !!