July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Iundwe Serikali ya mpito Z’bar’

Spread the love

BAADHI ya viongozi wa vyama vya siasi nchini wameshauri kuundwa kwa serikali ya mpito itakayoshirikisha kila chama kufuatia mgogoro wa kufutwa matokeo ya Zanzibar. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya Mkutano wa Baraza la Vyama vya Viasa wa kumuaga Rais Jakaya kikwete anayemaliza muda wakewamesema kuwa, ni vema serikali hiyo ikahusisha zaidi ya chama kimoja cha upinzani.

Mgombea Urais visiwani Zanzibar kupitia ADA TADEA, Juma Ally Hatibu ameshauri Rais Kikwete kuuvalia njuga mgogoro wa Zanzibar kutokana na kwamba unaweza kukuwa endapo katiba ya visiwa humo itapaoshindwa kufuatwa.

“Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imeboronga na haikuwajibika ipasavyo ndio sababu ya kuliingiza taifa kwenye mgororo huu,” amesema Hatibu.

Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima (AFP) ambaye alikuwa mgombea urais wa chama hicho visiwani Zanzibar, Sudi Said Sudi amesema kuwa, kipindi hiki ambacho nchi ipo kwenye mchakato wa kusubiri kurudiwa kwa uchaguzi, iundwe Serikali ya Mpito.

Amesema serikali hiyo haipaswi kuwa ya vyama viwili au kimoja cha siasa, hata hivyo ameridhia kufutwa kwa uchaguzi huo kutokana kwa madai ya kasoro zake.

“Mimi kwa upande wangu nimeona kuwa uchaguzi ulikuwa una mapungufu mengi ikiwa kuna watu ambao wamekutwa wakiwa wana kura feki, kupigana kwa wajumbe wa ZEC pia kuonekana kwa watu ambao si mawakala wala si wasimamizi wa uchaguzi ndani ya vituo,” amesema Sudi.

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia Makini, Muhammedi Abdullah amesema kuwa, kwa mujibu wa katiba kifungu cha 28(1) kinaeleza kwamba ukumo wa Rais kutoka madarakani ni mpaka rais mpya aapishwe.

Ameshauri kuwa rais aliyekuwepo madarakani hatakiwi kuondoka mpaka apatikane rais mwengine.

Kwa upande wake aliyekuwa Mgombea urais wa Chama cha TLP, Maximullan lyimo amesema kuwa ameshindwa ambapo ameitaka serikali mpya kuunda serikali isiyokuwa na itikadi ili kujileta maendeleo katika taifa.

Mkutano huo uliandaliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa kupitia Baraza la Wanasiasa nchini.

error: Content is protected !!