August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Itikadi zavuruga Chadema, CCM Segerea

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Migombani, Japhet Kembo (kushoto) akimsikiliza Mwanasheria Idd Msanga.

Spread the love

ITIKADI za kisiasa zimetajwa kuzorotesha kasi ya maendeleo katika Mtaa wa Migombani, Jimbo la Segerea, mkoani Dar es Salaam, anaandika Pendo Omary.

Changamoto hiyo inakuja baada ya 22 Januari, mwaka jana kuapishwa kwa Japhet Kembo (Chadema), kuwa mwenyekiti mpya wa serikali ya mtaa huo.

Akizungumza na MwanaHALISI Online mapema leo, Kembo anasema “changamoto kubwa ninayokabiliana nayo katika kutekeleza ahadi zangu nilizoahidi wakati wa kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2014, ni baadhi ya watu kutumia utofauti wa itikadi za kisiasa kukwamisha utekelezaji wa ahadi zangu.”

“Wapo baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi katika mtaa wangu hawataki kuchangia au kushiriki katika shughuli za maendeleo. Taarifa ninazozipata ni kwamba wanataka maendeleo katika mtaa wetu yakwame ili wananchi wasinipe nafasi ya kuongoza tena katika uchaguzi ujao,” amesema Kembo.

Kembo anasema wakati anagombea nafasi hiyo, aliahidi kuboresha usafi wa mazingira, ofisi ya serikali ya mtaa kutoa huduma bure bila malipo, kuitisha mikutano ya wananchi, kuboresha miundombinu na kuimarisha ulinzi.

“Mpaka sasa utekelezaji wa ahadi zangu unaendelea vizuri. Najivunia kuboresha usafi. Tayari mkandarasa wa kuzoa taka kwa kila nyumba kuchangia Sh 10,000 kwa mwezi ambaye ni Juza General Suppr ameanza kazi. Tumeboresha barabara inayoanzia Oil Com hadi Seminari na sasa nipo kwenye mchakato wa kuhakikisha barabara ya Mega hadi Pazi inaboreshwa,” amesema Kembo.

Pia, amesema tayari amefanikiwa kuanzisha vikundi viwii vya ulinzi shirikishi ambavyo vinafanya kazi ya kuhakikisha wakazi na wageni wanaoingia katika mtaa huo wapo sarama pamoja na mali zao huku kila nyumba ikichangia Sh. 10,000 kwa mwezi.

error: Content is protected !!