January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Itigi yatengewa 1.3/- bilioni za umeme

Mafundi Umeme wakiwa kazini

Spread the love

SHILINGI 1.28 bilioni zimetengwa kwa ajili ya kupeleka umeme katika kijiji cha Mwamagembe, Tarafa ya Itigi mkoani Singida, Bunge limeelezwa. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga amesema mradi huo utanufaisha vijiji vya Kalangali, Kiyombo, Madole Tisa, Kitumbi, Mwamagembe na Mwamalugu.

Alisema kazi za mradi huo zitahusisha ujenzi wa njia ya umeme ya msongo wa kilovoti 33 umbali wa kilomita 65, ujenzi wa njia ya umeme ya msongo wa kilovoto 0.4 umbali wa kilomita 8.5, ufungaji wa transfoma 16 na kuwaunganishia umeme wateja wa awali wapatao 227.

Amesema hadi kufikia sasa utekelezaji umefikia asilimia 25 na mkandarasi anaendelea kufanyakazi katika vijiji vya upande wa wilaya ya Sikonge.

Kitwanga alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Manyoni Magharibi, Paul Lwanji (CCM), ambaye alitaka kujua ni lini mpango huo utetekelezwa ili wananchi wa Mwamagembe wapate umeme kabla ya Juni, 2015 kama ilivyoahidiwa.

error: Content is protected !!