SERIKALI ya Israel imekamata raia wake wanne na kuwafungulia mashitaka kwa kosa la kumpiga mhamiaji kutoka Eritrea na kumuua.
Taarifa kutoka kwenye nchi hiyo zinaeleza kwamba, utetezi wa waisrael hao umeeleza kuwa walichukua hatua hiyo baada ya kumdhania mtu huyo kuwa ni mpiganaji wa kiarabu.
Raia huyo wa Eritrea alitajwa kwa jina la Habtom Zerhom alikutwa kwenye kituo cha basi wakati ambao raia mmoja wa Palestina aliposhambulia na kumuua askari wa Israel.
Kutokana na hali hiyo, Walinzi wa Usalama waliokuwepo kwenye shambulio hilo wanaeleza kumdhania Zerhom kuwa ni mshirika wa mshambuliaji huyo na hivyo kulazimika kumpiga risasi.
Pamoja na maumivu aliyoyapata Zerhom kutokana na kupigwa risasi, kundi la watu liliibuka na kuanza kumshambulia kutokana na hasira walizokuwa nazo. Hata hivyo, Zerhom alifariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata.
More Stories
Waziri mkuu Uingereza agoma kujiuzulu
Rwanda, Congo wakubaliana kumaliza tofauti zao
10,000 wafariki vita ya Urusi, Ukraine