May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Israel yaanza mashambulizi Gaza

Spread the love

 

JESHI la Israel limefanya mashambulizi ya kijeshi baada ya kudai, Palestina kushambuliwa nchi hiyo kwa maguruneti. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Jeshi hilo limeeleza, limelenga kundi la waasi la Hamas ambao ni chama tawala cha siasa cha Palestina, na kwamba mashambulizi hayo yamelenga kambi mbili za ‘waasi’ hao.

Israel imeeleza, mashambulizi ya Palestina katika ardhi ya Israel, hayajasababisha madhara yoyote.

Hamas imeeleza, pamoja na mashambulizi ya Israel kuendelea, eneo la Gaza litaendelea kupiginiwa na Wapalestina mpaka mwisho wa uhai wao, akisistiza nchi hiyo haijafanya mashambulizi Israel.

Israel imeweka vikwazo mbalimbali vya kuingia Palestina kupitia barabara, baharini pamoja na viwanja vya ndege. Mgogoro wa ardhi kati ya Israel na Palestina ulianza mwaka 1967.

error: Content is protected !!