Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Michezo Ishu ya Mukoko na Kaizer Chiefs iko hivi
Michezo

Ishu ya Mukoko na Kaizer Chiefs iko hivi

Mukoko Tonombe, mchezaji wa klabu ya Yanga
Spread the love

 

MARA baada ya tetesi za Mokoko Tonombe kutakiwa na klabu ya Kaizer Chiefs inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini uongozi wa klabu hiyo umefunguka na kueleza kuwa timu hiyo ambayo ni kongwe barani Afrika walikuwa na nia ya kumsajili mchezaji huyo kabla ya kuja Yanga lakini sio sasa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mukoko ambaye alisajiliwa Yanga 2020 akitokea klabu ya As Vita Club inayoshiri Ligi ya Congo kwa mkataba wa miaka miwili mpaka mwaka 2022.

Akitoa ufafanuzi huo Afisa Habari na muhamasishaji wa klabu ya Yanga Antonio Nugaz amesema kuwa  uongozi wa Kaizer Chief kupitia Mkurugenzi mkuu wa tathimini, usajili wa wachezaji na maendeleo ya klabu Walter Steenbok walibainisha wazi kuwa waliwahitaji Mukoko na Tuisila Kisinda kabla ya kuja Yanga na sio ka kipindi hiki.

Kiongozi huyo wa kaizer Chiefs alisema hayo wakati alipoitembelea klabu ya Yanga jijini Dar es Salaam hivi karibuni na kukutana na uongozi wa mabingwa hao wa kihistoria wa ligi Kuu bara na kuweka bayana juu ya kuhitaji wachezaji hao.

“Tuliwafutilia Mukoko na Tusila wakiwa AS Vita, tulipoenda tena tukaambiwa wamechukuliwa na Yanga, nilitaka kujua mbinu zenu za Scouting, japo Yanga hamna scouting team lakini niwapongeze kwa jicho lenu kwa Wachezaji hawa ambao hata sisi tuliwaona,” alisema Steenbok.

Viongozi hao wa Kaizer Chiefs walifanikiwa pia kukutana na baadhi ya watendaji wa klabu ya Yanga akiwemo Mkurugezni wa uwekezaji wa GSM mabo ni wadhamini na wafadhili wa klabu hiyo Mhandisi Hersi Said pamoja na mshauli wa klabu hiyo raia wa Afrika kusini Senzo Mbatha.

Aidha kwa mujibu wa Nugaz katika maongezi hayo uongozi wa Kaizer chief uliwapongeza klabu ya Yanga kwa kuwa na jicho zuri kwenye usajili wa wachezaji kiasi cha kuwaona wachezaji ambao hata wao waliwavutia wakiwa Congo na klabu ya As Vita Club.

Pia msemaji huyo alikazia kwamba kaizer Chief hawana nia yoyote ya kuwachukua wachezaji hao kwa sasa kiasi cha kutengeneza hofu kwa mashabiki wa klabu hiyo na kudai kuwa waliofanya hivyo walikuwa na makusudi ya kuzua taflani ndani ya klabu hiyo.

Mukoko ambaye mpaka hivi sasa amehusishwa na kutakiwa na klabu nyingi mara baad ya kuonesha kiwango cha hali ya juu toka alipojiunga na Yanga katika michezo mbalimbali aliocheza ya kimashindano.

Kiungo huyo ambaye alijiunga Yanga kama mbadala wa Papy Kabamba Tshishimbi ambaye alitimka klabuni hapo mara baada ya msimu wa 2019/2020 kukamilika na kujiunga na klabu ya As Vita ya nchini Congo ambayo hivi Jumamosi ya Aprili 3, 2021 itakuwa na kibarua dhidi ya Simba kwenye mchezo wa klabu bingwa.

Wachezaji hao wawili toka wajiunge Yanga wamekuwa muhimili mkubwa hasa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo na kuisaidia kuiweka kileleni kwenye Ligi Kuu mpaka hivi sasa.

Kwenye ligi Kuu bara Mukoko amefanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora mwezi oktoba mwaka jana mara baada ya kuwabwaga mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube na  mshambuliaji wa Gwambina FC, Meshack Abraham aliongia nao fainali.

Licha ya kucheza katika eneo la kiungo wa ulinzi Mukoko amekuwa na mchango mkubwa kwa kufunga mabao na kutoa pasi za mwisho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!