Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ‘Ishu’ ya Jokate: JPM awapasua mbavu Kisarawe
Habari za Siasa

‘Ishu’ ya Jokate: JPM awapasua mbavu Kisarawe

Spread the love

RAIS John Magufuli amewataka wakazi wa Kisarawe ‘kuchangamkia fursa’ ya kumoa Jokate Mwegelo, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Akizungumza katika uzindua mradi wa maji wilayani Kisarawe katika Mkoa wa Pwani leo tarehe 28 Juni 2020, Rais Magufuli ameonesha kushangazwa na wanaume wa wilaya na mkoa huo kushindwa kumuao binti huyo kwa kuwa, hana mume mpaka sasa.

“Mkuu wa Wilaya (Jokate) amefanya kazi ya kuondoa zero, hajaolewa lakini hamjamuoa, mnamuangalia tu hapa. Ndio shida ya Wazaramo,” kauli hiyo ya Rais Magufuli ilifuatiwa na kicheko huku kikubwa kilichotoka kwa wananchi waliohuzuria uzinduzi huo.

Rais Magufuli amesifu baadhi ya watendaji wake waliotoka kwenye wilaya hiyo akiwemo Suleiman Jafo, Waziri wa TAMISEMI kwamba amefanya kazi vizuri.

“Nitashangaa sana kama aliyofanya Jafo hamtayaona, mwenye macho haambiwi tazama,” amesema.

Akizungumzia mradi huo, Rais Magufuli amewataka wakazi wa wilaya hiyo kuutunza ili uwanufaishe kwa muda mrefu.

“… nimekuja kuzindua mradi, wanakisarawe tunzeni mradi huu, mradi huu umetumia fedha zenu, msiyaache maji yakawa yanamwagika. Maji ni uhai,” amesema na kuongeza:

“Mliteseka sana miaka ya nyuma, mama ameondoka mapema anasema anaenda kuchota maji, kumbe ana misheni zake. Wakati huu, huo mchezo haupo, mambo yamebadilika. Maji yapo.”

Rais Magufuli amewataka wakazi wa wilaya hiyo kudumisha Amani iliyopo sasa, na kwamba wasitake warejee miaka ya nyumba ambapo wilaya hiyo ilikuwa kichaka cha wahalifu.

“Nitoe witi kwa wanakisarawe kuendelea kudumisha amani na utulivu, amani ndio msingi wa maendeleo. Miaka mitatu iliyopita, wilaya hii ilitumika kama maficho ya wahalifu. Niwahisi hali hiyo isirudie.

“Wakati sijaingia madaakani, ni mkoa ambao ulikuwa haujatilia sana. Wahubiri wote masheikh mapadri wote wanahubiri amani,” amesema.

Pia ameta wito kwa wakazi hao na Tanzania kwa ujumla katika uchaguzi mkuu ujao kuchagua viongozi watakaotetea na kujali maendeleo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!